Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, October 15, 2014

AGNESS TRUST WAFANYA MAHAFARI YA KIDATO CHA NNE ,YAWATAKA KUHESHIMU WAZAZI WAO KWA WAAGWA





 WANAFUNZI  WA AGNESS TRUST WAKIONESHA BURUDANI MBELE YA WAGENI RASMI


MKURUGENZI WA AGNESS TRUST AITOA NASAHA

Jumla Ya Wanafunzi 34 Wanatarajia Kufanya Mtihani Wa Kidato     Cha Nne Katika Shule Ya  Sekondari Agnes Trust Ambapo Pamoja Na Mambo Mengine Wanafunzi Hao Wametakiwa  Kwenda Kuwasaidia Wazazi Kufanya Kazi Za Mikono  Na Kuepukana Na Tabia Ya Kuzurula Na  Kushinda Vijiweni Wakati Wakijiandaa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Kwa Watakaofaulu.

Rai Hiyo Imetolewa Na Katibu Msaidizi Wa Tahosa Ambaye Ni Mkuu Wa Shule Ya Sekondari  Mpechi  Bwana Peter Mwavela Wakati Akiwa Mgeni Rasmi Katika Mahafari Ya Pili Ya Kidato  Cha Nne Ya Shule Ya Sekondari Agnes Trust  Ambapo Amesema Wazazi Wanatakiwa Kwenda  Kuwaendeleza Na Masomo Ya Ziada Wakati Wakisubiri Matokeo   Ili Wanafunzi Hao  Wasipate Muda Wa Kuzurula Mitaani.

Bwana  Mwavela Amesema Kuwa Halmashauri Ya Mji  Wa Njombe  Ina Jumla Ya Shule 27 Ambapo Shule Ya Sekondari Agnes Trust Imekuwa  Miongoni Mwa Shule Zinazofaulisha  
Vizuri  Na Kuwaomba Walimu Wa Shule Hiyo Kuendelea Na Jitihada Za Kuwalea Na 
Kufundisha Watoto Katika Misingi Ya Maadili Ya Kidini,Kielimu Na Ujasiliamali Ambao 
Umekuwa Ukifundishwa Kwa Wanafunzi Wa Shule Hiyo.

Aidha Bwana Mwavela Amekemea Tabia Ya Vijana Kujihusisha Na Matukio Ya Wizi  Na 
Ukiukaji Wa Maadili Kwa Kuvaa Mavazi Yasiyo Stahili Kwa Jamii Tofauti Na Waliofundishwa  Wakiwa Shuleni  Na Kusema Kuwa Wanatakiwa  Kusoma Kwa  Malengo Huku Wazazi  Wakiwalea    Kwa Maadili Mema Na Kukemea Tabia Mbaya Zitakazofanywa Na Wanafunzi  Hao Watakapo Kuwa  Nyumbani.

Kwa Upande Wake Mkurugenzi Wa Shule Ya Sekondari Agnes Trust  Bi.Agnes Temu  
Amewataka Wanafunzi Kwenda Kujishughulisha Nyumbani Kwa Kufanya Kazi  Kwani 
Amewafundisha Shughuli Mbalimbali Za Kijasilimali Na Kuwaheshimu Walezi Na Wazazi  Na  Kusema Kuwa Kwa Wale Yatima Hawatakiwi  Wanatakiwa Kuzitumia Mbinu Walizofundishwa  Shuleni Hapo Na Namna Ya  Kuishi Na Walezi Na Wazazi Kwa Kufanya Kazi Kwa Juhudi Na Kutii  Maagizo Ya Walezi Na Wazazi Wao.

Amesema Wahitimu Wanatakiwa Kujenga Tabia Njema Kwa Jamii , Kuwa Wabunifu Na 
Kwamba Watoto Wengi Wamekuwa Wakisingizia Kuwa Ni Yatima Jambo Ambalo Mkurugenzi  Huyo Amepingana Na Mawazo Hayo Kwa Kusema Wanafunzi Wengi  Wakitoka Shuleni   Huanza Kuendekeza Uzembe Nyumbani Kutokana Na Baadhi Ya Wazazi  Kutowafutilia  Jambo  Ambalo Baadhi Yao  Wanaingia Kwenye Matukio Ya Wizi Na Matumizi Ya Madawa Ya  Kulevya.


Akisoma Risala Kwa Niaba Ya Wanafunzi Wanaohitimu  Elimu Ya Kidato Cha Nne  Anitha 
Boniface Mayugi  Amewashukuru Walimu Kwa Kuwafundisha Taaluma Na Maadili Shuleni  
Na Kwamba Wanaomba Wastani Wa 45 Uongezwe Na Kufikia Wastani Wa Asilimia 55  Ili 
Kupata Wanafunzi Wenye Ufaulu Wa Juu Katika Mitihani Ya Kitaifa.

No comments:

Post a Comment