Wednesday, September 10, 2014
KAMISHNA WA KAMISHENI YA POLISI JAMII MUSSA ALLY MUSSA AWATAKA ASKARI WA KATA KUHAMIA MAENEO HUSIKA
KAMISHNA WA KAMISHENI YA POLISI JAMII MUSSA ALLY MUSSA AKIWASILI KATIKA OFISI ZA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE
WAKUU WA VITUO VYA POLISI NA MAOCD WA KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA NJOM,BE WAMEWASILISHA TAARIFA ZAO FUPI KWA KILA HALMASHAURI.
KAIMU KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE ACP FRANCO KIBONA AKIMKARIBISHA KAMISHNA WA KAMISHENI HUYO
KAMISHNA WA KAMISHENI YA POLISI JAMII MUSSA ALLY MUSSA AKITOA HOTUBA YAKE KATIKA UKUMBI WA POLISI MKOA WA NJOMBE
Kamishna wa Kamisheni ya polisi Jamii Nchini Mussa Ally Mussa amewaagiza wakuu wa polisi jamii wa kata kuhamishia makazi yao kwenye kata walizopangiwa ili kuzuiya matukio ya uharifu ambayo hutokea katika maeneo hayo.
Agizo hilo la Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii Nchini Mussa Ally Mussa amelitoa hapo jana wakati akizungumza na Wakuu wa vituo vya Polisi wa halmashauri za Wilaya Mkoani Njombe ikiwemo halmashauri ya Wilaya ya Makete,Ludewa,Wanging'ombe,Halmashauri ya mji wa Makambako,halmashauri ya mji Njombe na Wilaya ya Njombe.
Akizungumza na Askari hao Kamishna wa Kamisheni wa polisi jamii Huyo Mussa Ally Mussa amesema kuwa hatua hiyo imefuatia kuwepo kwa umbali wa kata zilizoko hapa Nchini ili hali Jeshi la polisi linakabiliwa na changamoto za kukosekana kwa vyombo vya usafiri jambo ambalo limepelekea jeshi hilo kushindwa kufika kwa wakati maeneo husika.
Aidha Kamishna wa Kamisheni wa hiyo amesema kuwa Askali atakaye pangiwa kata ya kusimamia anatakiwa kubuni mbinu mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa jamii katika musimu wa nmavuno juu kuhifadhi fedha zao katika taasisi za kifedha za benki Ambapo viongozi wa kata na vijiji wanatakiwa kuwajengea nyumba za kuishi askari hao.
Awali wakitoa taarifa mbalimbali za jeshi la polisi kwa kila halmashauri za mkoa wa Njombe wakuu wa jeshi la polisi kati wilaya hizo akiwemo OCD wa Wilaya ya Ludewa ASP Edward Emmanuel Mtailuki na mkaguzi msaidizi wa polisi taarafa ya Makambako Raphael B.Mlangwa wamesema jeshi la polisi limekuwa likikabiliwa na upungufu wa vyombo vya usafiri,uchache wa watumishi wa jeshi hilo Pamoja na silaha.
Akifunga kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa jeshi la polisi Mkoa wa Njombe kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani, Mkuu wa upelelezi mkoa wa Njombe ACP Franco A. Kibona Ameahidi kuyafanyia kazi yale yote yaliotolewa na Kamishna huyo na kuwataka askari kutekeleza maagizo hayo kwa kushikamana na jamii ili kuzuia uharifu usitokee kwa kushirikisha makundi mbalimbali ya viongozi na wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment