Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, August 15, 2014

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA MJINI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


   Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Njombe




 NAIBU AFISA UHAMIAJI MKOA WA NJOMBE ROSE MHAGAMA


 Pasipoti Nne za Baadhi ya Wahamiaji Hao Waliokamatwa Mjini Makambako







HAYO NI MAJINA YA WAHAMIAJI HAO HARAMU

  Hao Ndio Wahamiaji Haramu Wakiwa Katika Ofisi za Uhamiaji Mjini Makambako
HAWA NI WAHAMIAJI HARAMU WALIOKAMATWA MKOANI NJOMBE WAKIWA KWENYE GARI LA MIZIGO LILILOKUWA LIMEPAKIA MIFUKO YA SARUJI NA DEREVA WAKE ALIKIMBIA  NA ANAENDELEA KUTAFUTWA


Idara ya Uhamiaji Mkoani Njombe Kwa Kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoani Humo Linawshikilia Raia 21 Kutoka Nchini Ethiopia Kwa Tuhuma ya Kuingia Nchini Kinyume cha Sheria za Nchi.

Akizungumza Mara Baada ya Kukamatwa Kwa Raia Hao Katika Ofisi Ndogo za Uhamiaji Zilizopo Halmashauri ya Mji wa Makambako , Naibu Kamishina wa Uhamiaji Mkoa wa Njombe Bi. Rose Mhagama Amesema Raia Hao Wamekamatwa Agosti 14 Mwaka Saa  Mbili Usiku Eneo la Mashuja Mtaa wa Mjimwema, na Hapa Anaelezea .

Naibu Kamishina Mhagama Amesema Raia Hao Wamekamatwa Wakiwa Ndani ya Gari Aina ya Scania Iveco Yenye Namba za Usajili T 587 CSN Likiwa na  Tela Lenye Namba za Usajili T780 CHN Mali ya Everest Freght. LTD ya Jijini Dar Es Salaam Lilokuwa Limebeba Saluji.

Naibu Kamishna Huyo wa Uhamiaji Amesema Gari Hilo Lilikuwa Likitokea Mkoani Tanga Kuelekea Mkoani Njombe Ambapo Dereva wa Gari Hilo Aliyefahamika Kwa Jina Moja la Nyange Ametoroka, Huku Akiwaomba Wananchi Kuendelea Kushirikiana na Idara Hiyo Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na Biashara ya Kusafirisha Binadam.

No comments:

Post a Comment