Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, August 17, 2014

UWT MKOA WA NJOMBE WA TEUWA WALEZI


Mbunge  Filikunjembe na Mafulu  wakipongezwa  kwa  kuteuliwa  walezi wa UWT  Njombe
Dr Suzana  Kolimba wa  tatu kushoto  akipongezwa kwa mchango  wake  UWT
walezi  wa UWT  mkoa  wa NJombe mbunge wa  Ludewa  Deo  Filikunjombe ( kulia ) na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Lediana Mafulu wakipongezana kwa kuteuliwa  kuwa  walezi wa UWT mkoa wa Njombe
Mbali ya  Filikunjombe  kuendesha  harambee  hiyo  kwa  yeye  mwenyewe  kuchangia  milioni 10 kwa  ajili ya kuchangia  ununuzi wa gari hilo pia  mjumbe  wa bunge la katiba  ambae ni mchumi  wa   UWT mkoa wa  Njombe Dr  Suzana Kolimba alichangia  kiasi  cha Tsh milioni 5  katika  harambee  hiyo.
Akizungumza  baada ya  kuendesha  harambee  hiyo na  kusimikwa  kuwa  mlezi  wa  UWT  mkoa  wa Njombe  pamoja na mbunge Lediana Mafulu  Mng’ong’o  mbunge  Filikunjombe  alisema  kuwa  lengo la  kuchangisha  fedha  hizo ni kuiwezesha  UWT  Njombe  kuwa na gari  lake la kisasa  ambalo  litasaidia kuendesha shughuli  za  jumuiya  hiyo.
“Nilipopokea taarifa za kuteuliwa na Jumuiya yenu kuwa Mlezi, kwanza nilishituka, msituko nilioupata haukuwa wa kuogopa majukumu bali ulikuwa ni mshituko wa tafakuli niliyoifanya juu ya uzito na hadhi ya nafasi hii ya Ulezi, maana sisi sote tunaonekana katika sura ya Uongozi wa Taifa na dunia tumezaliwa na wanawake na asilimia kama 99% tumelelewa na wanawake. Kwa hiyo swali gumu nililokuwa najiuliza ni
namna gani ninaweza kuwalea watu wenye uzoefu mkubwa wa kulea watu kuanzia mimba, kuja mtoto hadi kufikia hatua akaweza kuwa rais au Waziri. Uzoefu huo wanao akina mama tena chini ya uangalizi na uvumilivu mkubwa. “
 Filikunjombe  alisema  kuwa anatambua vema nafasi na wajibu wa akina mama katika ujenzi wa CCM Imara, kama vile historia ya nchi yetu tokea Uhuru ilivyoainisha mchango mkubwa wa akina mama wakati wa kutafuta Uhuru wa nchi yetu, michango kama ya akina Bibi Titi Mohamed wakati wa harakati za Chama cha TANU kutafuta Uhuru wa Tanganyika. 
“Zaidi ya hilo taarifa za kiutafiti zinaonyesha kuwa kura nyingi za ushindi za CCM tokea tulipoingia kwenye mfumo wa Vyama vingi mwaka 1992  ni za Wanawake, maana  wanawake wanamsimamo, hawayumbi na wanajua wao ni Waathirika wa kwanza nchi inapoingia kwenye machafuko. “
Hata   hivyo  alisema kuwa moja  kati  ya  mkakati  wake kama  mlezi  wa  UWT  mkoa  wa  Njombe ni  kuona  mkoa  hao  unakuwa mkoa wa  pekee  kwa kutoruhusu  upinzani  kuchukua  nafasi
“ Kazi  yangu kama  mlezi  ni  kuhakikisha  naitumikia  vema  nafasi  hii na  kuhakikisha  kupitia  jumuiya  hii  mbengu mbovu ya  upinzani  ambayo  imejipachika katika  mkoa  wetu  inaondoka  haraka  iwezekanavyo na mwaka  2015  mkoa  wa  Njombe  wote  unakuwa na  wa CCM.
Huku  mchumi  wa  wilaya  hiyo  Dr  Suzana  Kolimba  mbali ya  kuchangia  kiasi  hicho  cha Tsh  milioni 5 kwa ajili ya  kuunga mkono  jitihada za  mlezi  Filikunjombe pia  alisema  kuwa  lengo lake kama mchumi  ni kuona mkoa  huo wa  Njombe  hasa  wanawake  wanaendelea  kuwa na uchumi imara .
Kwa  upande  wake  mlezi Mafulu  pamoja na kuipongeza  jumuiya  hiyo ya UWT kwa  kumteua  Filikunjombe nay eye  kuwa  mlezi  alisema kuwa  bado jumuiya  hiyo haikukosea   kuwateua  kwani  wao ni  miongoni mwa  watendaji  wazuri katika chama  hicho.
MWISHO

No comments:

Post a Comment