MWENYE SWETA NYEKUNDU NI FRED KADUMA BABA WA MICDADI FRED KADUMA AKIWA NYUMBANI KWAKE
MAMA WA KAMBO EDNA NYAGAWA AMBAYE NAYE AMESEMA AMECHOKA KUISHI NA MTOTO HUYO MWENYE ULEMAVU NA KWAMBA KWA KUWA SIYO MTOTO WAKE
MWENYEKITI WA KIJIJI CHA LUNGUYA VALENTINO MWELANGE AKIWA OFISINI KWAKE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Kauli hiyo Imetolewa na Kaimu afisa Ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe bi. Sarah Chambachamba baada ya wananchi wa kijiji cha Lunguya kulalamikia wazazi wa mlemavu huyo Fred Kaduma na Edna Nyagawa kumtumikisha kazi ngumu ikiwemo kuokota kuni polini ikiwa anaulemavu wa miguu na mikono.
Aidha bi.Chambachamba amesema kwa mujibu wa sheria ya walemavu ya mwaka 2010 inayosema jamii inawajibu mkubwa wa kutoa ulinzi kwa watoto wenye ulemavu walio katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali pindi Unyanyasaji,unyanyapa na
matendo mengine yanayokiuka haki za binadamu.
Bi.Chambachamba amesema kutokana na mlemavu huyo kunyanyaswa na kukataliwa na wazazi wake akiwemo baba yake mzazi bwana Fred Kaduma, Wazazi upande wa marehemu mama yake na Micdad Fred Kaduma wameamua kumchukua na Kumlea Mlemavu huyo wakati serikali ikiendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wazazi hao.
Wakizungumza majirani wa wazazi wa mtoto huyo wameelezea kusikitishwa na tabia ya wazazi hao ya kumnyanyasa kwa kumuadhibu na viboko hadi kumsababishia majeraha Ambapo matendo hayo yameanza kujitokeza baada ya kujenga nyumba mpya makambako na kutaka kuuza wanayoishi ambayo ilijengwa na marehemu mama wa mlemavu huyo.
Kwa upande wa wazazi wa mtoto mwenye ulemavu Ambao ni Fred Kaduma na Mke wake Edna Nyagawa wamesema kutokana na maneno yanayotolewa na majirani juu ya mtoto Micdad Fred Kaduma wamechoka kuishi naye kwa madai ameanza tabia za wizi na kujisaidia ovyo ndani ya nyumba Ambapo tabia hizo zimeanza
siku za hivi karibuni baada ya mlemavu huyo kusikiliza maneno ya majirani kuwa nyumba wanayoishi ni ya marehemu mama yake.
Viongozi wa Kijiji hicho akiwemo mwenyekiti bwana Valentino Mwelange na Afisa mtendaji wake Elphasi Lulimo wamekili kutokea kwa tatizo la wazazi hao kumnyanyasa mlemavu huyo na kuahidi kusimamia haki ya mlemavu huyo na dada yake kuwa nyumba yao haiuzwi hata kama watahamia makambako.
No comments:
Post a Comment