Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, August 14, 2014

BENJAMIN MKAPA AZITAKA JAMII ZA KIAFRIKA KUJIFUNZA ELIMU YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA


RAIS Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa amezitaka jamii nyingi za kiafrika kuwa na uelewa wa kutosha kuhusiana na mchango wa sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo nchini.

Mhe. Mkapa ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Jiolojia uliowakutanisha wataalam mbalimbali wa mambo ya jiolojia ulimwenguni akiwa ameongozana na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo pamoja na Naibu Waziri wake, Mhe. Stephen Masele.

Mhe. Mkapa ameeleza kuwa ni vema kwa wanasayansi ulimwenguni kujenga utamaduni wa kukutana mara kwa mara na kujadili mambo yanayohusu sayansi na teknolojia ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii ambazo zitatatua migogoro inayoweza kujitokeza baina ya nchi na wawekezaji.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania, Profesa Abdulkarim Mruma

akitoa hotuba yake fupi mbele ya wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Jiolojia

uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Wajiolojia Afrika Profesa Aberra Mogessie akiwahutubia wajumbe

waliohudhuria Mkutano wa Jiolojia uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa

J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment