Mkuu wa Wilaya Ya Njombe Bi.Sarah Dumba amewaagiza maafisa na Waratibu Elimu Wilayani Humo kuhakikisha wanatembelea shule zote za msingi na sekondari na kuwachukulia hatua kali za kidhamu walimu wote watakaobainika kuhusika na zoezi la kuwarudisha nyumbani wanafunzi kwa kukosa michango.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Uplands fm Kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya huyo kupata ufafanuzi kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kulalamikia kurudishwa nyumbani wanafunzi AMBAO michango ya shule licha ya serikali kupiga marufuku walimu kuwarudisha nyumbani wanafunzi badala yake zitafutwe mbinu za kuwawajibisha wazazi.
Aidha Bi. Dumba amewapongeza madiwani na watendaji wa kata na vijiji kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchangia michango ya chakula shuleni na kuwataka kuhakikisha wanafuatilia walimu wanaowarudisha wanafunzi nyumbani kwa kukosa michango na Na kuweka utaratibu mzuri wa kukusanya michango hiyo ili wanafunzi wapate elimu bora huku wito ukitolewa kwa wazazi kuchangia chakula hicho .
Bi.Dumba amesema wananchi wanatakiwa kuhakikisha kila mchango unaopelekwa shuleni unakatiwa stakabadhi ya malipo ili kuepukana na ubadhilifu unaoweza kujitokeza ambapo changamoto za kukosekana kwa stakabadhi wachukue hatua za kufuata sehemu husika.
Kaimu afisa elimu wa shule za Sekondari wilaya ya Njombe Christopha Haule amesema taarifa hizo Za kurudishwa nyumbani wanafunzi wa shule wilayani humo hazijamfikia na kwamba anatarajia kutembelea shule zote ili kubaini tatizo hilo na kuchukua hatua kwa baadhi ya walimu wakuu waliokaidi agizo la serikali la kutorudisha nyumbani wanafunzi waliokosa michango ikiwemo shule ya sekondari Ikuna.
Akijibu malalamiko ya wananchi wa kata ya Ikuna ya kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wasiyo timiza michango kaimu mkuu wa shule ya Sekondari Ikuna bi.Rose mary Mhagama amekili kuwarudisha baadhi ya wanafunzi nyumbani na kwamba hatua hiyo imetokana na makubaliano ya kwenye kikao cha wazazi kilichoazimia kurudishwa nyumbani wanafunzi ikiwa wazazi wamekanusha haja hiyo.
Jobu Fute ni Afisa mtendaji wa kata ya Ikuna ambae amekili kupata malalamiko toka kwa wananchi juu ya kurudishwa nyumbani kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Ikuna na kwamba uongozi wa kata hiyo ulikwisha zuia wanafunzi kutorudishwa nyumbani kwa kukosa michango huku akisema anashangazwa kwa hatua inayofanywa na walimu hao na kuahidi kukutana na uongozi wa shule hiyo kujadili suala hilo.
Awali wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi wa vijiji vya kata hiyo wakaweka mambo hadharani juu ya kurudishwa nyumbani wanafunzi wa shule hiyo na kwamba serikali imekuwa ikipiga marufuku kuwarudisha watoto lakini walimu hao wamekaidi agizo la serikali..
No comments:
Post a Comment