RHODA MAHAVA NI MUWEKA HAZINA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKISOMA TAARIFA YA FEDHA ,MBELE YA MADIWANI
MADIWANI WA HALMASHAURI WAKIJADILI MADA MBALIMBALI ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA KATA ZAO
JULIUS SALINGWA NI DIWANI WA KATA YA KIDEGEMBYE AKIZUNGUMZA
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA AKISOMA MUHTASARI WA MKUTANO ULIOPITA
MAKAMU MWENEYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE AKITETA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
PIKIPIKI ZILIZOKABIDHIWA KWA KATA MBILI MTWANGO NA MATEMBWE ZILIZOTOLEWA NA SHILIKA LA TASSF KAMA ZAWADI KWA USHINDI WA USAFI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Licha ya Jitihada Kubwa Zilizofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya
Njombe za Kuongeza Ajira Kwa Watumishi Wapya Mara Baada ya
Kupata Kibali Cha Ajira na Kufanikiwa Kuajiri Watumishi 177 Kwa
Mwaka 2013/2014 Lakini Bado Inakabiliwa na Upungufu wa Watumishi
156.
Kutokana na Hali Hiyo Halmashauri Hiyo Imeendelea Kujiwekea
Mkakati wa Kufuatilia Vibali Vya Ajira za Watumishi Wengine Ili
Ifikapo Disemba 31 Suala Hilo Liwe Limefanikiwa.
Akitoa Taarifa Kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Njombe Kwenye Kikao Maalumu cha Madiwani Cha Kujadili Taarifa
za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Mweka Hazina wa
Halmashauri Hiyo Bi.Rhoda Mahava Amesema Kuwa Halmashauri Hiyo
Imelazimika Kuajiri Watumishi Wapya wa Sekta Mbalimbali Baada ya
Kupewa Kibali na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Bi.Mahava Amesema Kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Ilipaswa
Kuwa na Watumishi 2107 Ili Kukidhi Matakwa ya Upungufu wa
Watumishi Katika Halmashauri Lakini Baada ya Taarifa ya Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Kubaini Tatizo Hilo Iliagiza
Kutolewa Kwa Ajira Kwa Watumishi Hao Jambo Ambalo Hadi Sasa
Imekwisha Ajira Jumla ya Watumishi Hao 177 Kati ya 333
Waliotakiwa Kuongezwa.
Pamoja na Mambo Mengine Halmashauri Hiyo Imerejesha Hazina Kuu
Zaidi ya Shilingi Milioni 50 Fedha Ambazo Hazikutumika Kama
Mishahara ya Watumishi Mbalimbali Wakiwemo
Waliostaafu,Watoro,Waliofariki na Walioacha Kazi Jambo Ambalo ni
Kinyume Cha Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Serikali za Mitaa ya
Mwaka 2009.
Akijibu Baadhi ya Maswali ya Madiwani Katika Kikao Hicho
Waliotaka Kujua Hatua Zinazochukuliwa Dhidi ya Ubadhilifu
Unaotokana na Uzembe wa Baadhi ya Watumishi waSerikali
Mwakilishi wa Mkaguzi Mkuu Mkoa wa Njombe Bwana Nyigane Mahende
Amesema Kwa Kawaida Taarifa Zinawasilishwa Bungeni Kwa
Majadiliano Ambako Ndiko Hatua Zaidi Huchukuliwa na Wabunge
Kutoa Maagizo Kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment