KATIBU WA MKOA WA CHAMA CHA WALIMU MKOA WA NJOMBE BWANA TWEEDSMA ZAMBI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI LEO OFISINI KWAKE
HAWA NI BAADHI YA WALIMU WA KUTOKA WILAYA ZA MKOA WA NJOMBE WAKIWA NJE YA OFISI YA CWT MKOA WA NJOMBE
HAWA NI BAADHI YA WALIMU WAKIHOJIANA NA WAANDISHI WA HABARI
Chama cha Walimu mkoa wa Njombe Leo kimetoa tamko kuhusu mpango
wa serikali wa kupunguza mafao ya watumishi wakistaafu baada ya
chama hicho kujadili kwa kiina rasimu ya mapendekezo ya Wizara
ya kazi na ajira kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya
mifuko ya jamii-SSRA ya mafao ya wastaafu wanachama wa mifuko ya
pesheni kwa watumishi wa umma PSPF na watumishi wanachama wa
LAPF.
Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kikao cha walimu bwana
Shabani Ambindwile Mwabunguru kilichowakutanisha wenyeviti na
makatibu wa vyama vya walimu wa wilaya za Mkoa wa Njombe
ambacho kililenga kujadili juu ya kupunguzwa kwa mafao hayo na
kusema CWT Mkoa wa Njombe kimeazimia kupinga mpango huo ambao
unalenga kuwadhulumu walimu na wafanyakazi wengine mafao ya
kustaafu kama utapitishwa na kutungiwa sheria.
Aidha bwana Mwabunguru amesema kuwa maeneo yanayopingwa na chama
hicho ni pamoja na kupunguza malipo ya pesheni ya mkupuo
yanayolipwa na mifuko ya PSPF na LAPF kutoka asilimia hamsini ya
sasa hadi kufikia asilimia 33.3 ya mshahara wa mwezi wa
mtumishi kabla ya kustaafu.
Akizungumza kwa upande wake katibu wa chama cha walimu mkoa wa
Njombe bwana Tweedsma Zambi amesema Chama hicho kimepinga kwa
nguvu zote rasimu hiyo na kwamba endapo serikali itashindwa
kupokea mapendekezo hayo ya walimu watakubaliana na hoja za
kwamba kuna serikali isiyo sikivu na inaweza kusababisha madhara
kwa jamii na wanafunzi Nchini.
Kwa upande wao makatibu na wenyeviti wa vyama vya walimu kutoka
Wilaya za mkoa wa Njombe wamesema hawakubaliani na mapendekezo
ya serikali juu ya kupitisha kanuni ya kupunguza mafao kwa
wastaafu na kwamba wameshangazwa kuona hawajashirikishwa katika
maamuzi ya utaratibu mpya unaotarajiwa kuanzishwa.
No comments:
Post a Comment