Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, August 8, 2014

KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA SOUTH WEST TANGANYIKA YAFANYA UCHAGUZI WA ASKOFU MKUU WA NANE

 HILI NI KANISA LA ANGLIKANA NJOMBE NA HAPA NDO WANNATOKA BAADA YA KUHITIMISHA ZOEZI LA UCHAGUZI


 KATIBU MKUU WA KANISA LA ANGLIKANA TANZANIA MCH.CANON DICKSON CHILONGANE AKIWA MJINI NJOMBE


KATIBU WA SINOD YA SOUTH WEST TANGANYIKA PAGRE LAMRCK LUOGA AKIZUNGUMZA MARA BAADA YA UCHAGUZI HUO

Na Michael Ngilangwa

Viongozi na Baadhi ya Waumini Kutoka  Kanisa la Anglikani Dayosisi ya South West Tanganyika Mkoani Njombe Hii Leo Wamemchagua Padrii Canon Methew Mhagama Kuwa Askofu Mkuu wa Nane wa Dayosisi Hiyo.

Akizumza na Waandishi wa Habari Mara Baada ya Kutangaza Matokea Hayo, Msimamizi wa Uchaguzi Huo Katibu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Mch.Canoni Dickson  Chilongane Amesema Zoezi la Uchaguzi Limefanyika Kwa Amani na Utulivu na Kuzingatia Taratibu Zote Tofauti na Chaguzi Zilizopita Zilizokuwa na Vurugu , na Hapa Anaeleza.

Aidha Mchugaji Dickson  Chilongane Amesema Uchaguzi Huo Umefanyika Kufatia Kifo cha Aliyekuwa wa Saba wa Dayosisi Hiyo Marehemu John Andrew Simalenga Aliyefariki Mwaka 2013  , na Kwamba Askofu Huyo Mpya Canon Methew Ataapishwa Oktoba Mwaka Huu.

Kwa Upande Wake Katibu wa Sinodi ya South West Tanganyika Padre Lameck Luoga Amewaomba Waumini wa Kanisa Hili Kuendelea Kudumisha Amani na Upendo Pamoja na Kushirikiana na Viongozi wa Kanisa na Dayosisi Hiyo.



Padre Luoga amewataka wakristo wa kanisa hilo kuendelea kudumisha amani na upendo katika kanisa kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa kanisa hilo katika kulitangaza neno la Mungu  na kukemea tabia ambazo hazimpendezi Mungu.

Nao Baadhi ya Waumini Walioshiriki Katika Uchanguzi Huo Wameushukuru Uongozi Kanisa la Anglikani Dayosisi ya South West Tanganyika Mkoani Njombe na Kusema Kuwa Kupatikana Kwa Kiongozi Huyo Kutasidia Kuharakisha Utekelezaji wa Miradi ya Kiuchumi ya Kanisa Hilo, Kama Wanavyoeleza.

Askofu Canoni Methew Mhagama amepita kwa kishindo baada ya kuwashinda  aliogombea nao ambao ni Padri  Raphael Galang'ula na Canoni John Kwetu ambao waliwania nafasi hiyo ya Uaskofu  Dayosisi ya  South West Tanganyika.


Uchaguzi huo umekuja Kufuatia Askofu Aliyekuwa Akiliongoza Kanisa Hilo Askofu wa saba John Andrew Simalenga Kufariki Dunia mwaka 2013  na kwamba Taratibu zote za uchaguzi zimefuatwa kwa kuwashirikisha waumini wa kutoka sehemu mbalimbali za dayosisi hiyo kushiriki katika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment