Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, July 31, 2014

Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Mahenge azindua tovuti ya mabadliko ya tabia nchi.

Mheshimiwa      Eng  Dkt. Binirithi S.  Mahenge
(mbunge)  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa  Rais (mazingira) azindua tovuti ya mabadiliko ya tabia  nchi. Katika hotuba yake fupi ya uzinduzi wa tovuti hiyo,
aliyoandaliwa kwa ufadhili wa serikali ya Denmark Mh. Binirithi  Mhenge amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi huangaliwa kwa muda wa miaka 30 hivyo kwa kipindi hiki chote kumekuwa na madhara mengi yatokanayo na athari za mabadiliko ya tabia Nchi ikiwa ongezeko
la joto, kina cha bahari kuongezeka pamoja na ongezeko la majanga ya mvua
zisizo na viwango,  kutoka na shughuli za binadamu katika uzalishaji hasa viwanda vikubwa





Alisema kwa tovuti inayozinduliwa ina umuhimu mkubwa kwani
inaelezea maeneo ya hali ya mabadiliko ya tabia
nchi na juhudi za serikali katika kukabiliana na athari zinazoletwa na
mabadiliko hayo.


“ziko sababu za kuungana na wenzetu ili kuondoa      tatizo hili la mabadiliko ya nchi ambapo
tovuti hii WWW.climatechange.go.tz
inatuunganisha na tovuti mbali mbali katika kupunguza gesi joto hapanchini pia
inaelezea fursa zilizopo katika miradi na program mbali mbali. Alisisitiza”





Alibaini kuwa tovuti hii itachangia kwa kiasi kikubwa
kuongeza uelewa na weledi kuhusu mabadiliko ya tabia  nchi nchini kwa wananchi na wadau kwa ujumla.


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt. Eng Binilith Satano Mahenge akizindua rasmi tovuti ya mabadiliko ya tabianchi itakayotumika kutoa taarifa mbalimbali za utunzaji wa Mazingira.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Mh. Dkt.
Eng Binilith Satano Mahenge (wa kwanza kushoto) akizungumza na wandishi wa
habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mkutano wa  Ofisi ya Makamu wa Rais leo jijini Dar es
Salaam, wakati wa uzinduzi wa "tovuti ya mabadiliko ya tabianchi" huku
akieleza malengo ya tovuti hiyo. kushoto ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Bw. Julius Ningu.


 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula (wa kwanza kushoto) na Mkuu Msaidizi wa Chuo cha SUA Prof. Gerald Monella wakisaini mkataba wa uwanzishwaji wa kituo cha Taifa cha kukusanya na kuratibu takwimu za hewa ukaa  uliofanyika katika ukumbi wa mkutano Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.



 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Sazi Salula wakipeana Mkataba na mkuu msaidizi wa wa chuo cha kilimo SUA Prof. Gerald Monella baada ya kusaini.

No comments:

Post a Comment