RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA PANDAMBILI MKOANI DODOMA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya
Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Rehema Nchimbi kufuatia ajali iliyotokea tarehe 30 Julai, 2014 katika eneo la
Pandambili, Wilayani Kongwa na kuua watu wapatao 18.
Katika ajali hiyo, watu 13 walifariki katika eneo la ajali, na majeruhi wapatao 56
walifikishwa hospitalini. Kati ya majeruhi hao hadi sasa waliolazwa ni 30 na
wengine wameruhusiwa baada ya kupata matibabu.
Rais amemuomba Dkt. Nchimbi kumfikishia rambirambi zake za dhati kwa ndugu na jamaa
waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, na kuwapa pole majeruhi wote na
kuwatakia kupona haraka ili warejee kwenye shughuli zao za kila siku.
“ Natoa Pole za dhati kwa wale wote walioondokewa na wapendwa wao katika ajali hii na pia
kuchukua nafasi hii kuwapa pole majeruhi wote na kuwaombea kupona haraka na
kurudi katika shughuli zao za kila siku”. Rais amesema katika salamu zake kwa Mkuu wa
Mkoa wa Dodoma.
“Hakika ni
jambo la kusikitisha sana kuondokewa na wananchi wetu katika ajali , natoa wito
wangu kwa madereva wote na wote wanaotumia vyombo vya moto kuwa makini wanapokuwa
barabarani “. Rais amesema na kuongeza kuwa;
“Kila dereva anaetumia chombo cha moto, ana wajibu wa kulinda maisha yake na ya watumiaji wengine kwa kuwa makini na muangalifu awapo barabarani, kwani ajali hizi zinarudisha nyuma maendeleo ya taifa na ya wananchi kwa ujumla” Rais amesema na kuvitaka vyombo vya ulinzi na
usalama barabarani kutolegeza kamba katika kuwachukulia hatua madereva wasio makini na wazembe wakati wote”.Rais amesisitiza.
Taarifa kutoka Mkoani Dodoma zinasema ajali hiyo ya jana (30 Julai, 2014) ilisababishwa na
Lori ambalo lilitaka kupita lori jingine na hivyo kwenda kugongana uso kwa uso na Basi la Moro Best lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Imetolewa na;
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es
Salaam.
30
Julai, 2014
No comments:
Post a Comment