Tuesday, July 29, 2014
WANANCHI WATAKIWA KUTOA TAARIFA ZA MAOVU PAMOJA NA MIGOGORO INAYOWAKABILI KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA MUJATA
MSHAURI WA MUUNGANO WA JAMII TANZANIA MUJATA NYANDA ZA JUU KUSINI BWANA KAYEMBA MPELEKA AKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WAJUMBE
HAWA NI BAADHI YA WAJUMBE WA MUJATA
KATIBU MUJATA MKOA WA NJOMBE MICHAEL KILANGO AKIZUNGUMZA NA NA WAJUMBE
Wananchi Mkoani Njombe Wametakiwa Kutoa taarifa kwa wakati kwa viongozi wa serikali na Asasi zisizo za kiserikali ambazo ni pamoja na MUJATA ambayo imeundwa ili kusaidia kutatua migogoro na kero zinazojitokeza ikiwemo ujambazi,Rushwa na Ukiukwaji wa haki za binadamu.
Hayo yamesemwa na Mshauri wa Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA bwana Kayemba Mpeleka wakati akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa Asasi hiyo kuhusiana na Kuungana na kupambana dhidi ya maovu yanayoikabili jamii ikiwemo Rushwa, Migogoro ya ardhi,imani za kishirikina na matatizo mengine ambayo ni chanzo cha uvunjifu wa sheria kutokana na kununuliwa kwa haki jambo ambalo linawakandamiza Wanyonge.
Aidha bwana Mpeleka amesema lengo la kuanzishwa kwa Muungano huo wa MUJATA hapa nchini ni kutaka kufanya kampeni dhidi ya maovu na kuhamasisha serikali,taasisi za kidini,na mashirika mbalimbali ili kuhakikisha haki inatendeka kwa jamii na kuleta amani na Utulivu ikiwa Rushwa ndiyo kilio kwa baadhi ya jamii masikini.
Kwa upande wake Katibu wa Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA mkoa wa Njombe bwana Michael Kilango amesema kuwa Wilaya ya Njombe imekuwa na Matukio mengi ya Migogoro ya Ardhi,mahusiano ya wanandoa pamoja na Imani za Kishirikina ambapo MUJATA imeshiriki kikamilifu kutatua Kero hizo ambazo zinaikumba jamii.
Wakizungumza Mara baada ya kufahamu lengo la Kuundwa kwa Muungano wa Jamii Tanzania MUJATA, Wajumbe wa Muungano huo wameshukuru kwa uwepo wa taasisi hiyo na kwamba watashirikiana kikamilifu ili kutatua kero mbalimbali ambazo zimekuwa ni kikwazo katika maendeleo Huku Rushwa ikitajwa kuwa ni kikwazo kikubwa cha kuwanyima haki wanyonge.
Asasi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na kuunganisha jamii kwa lengo Kuzuia na Kupambana na Maovu yanayoikumba jamii Nchini MUJATA imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na serikali katika kupambana na kero mbalimbali zinazoikabili jamii mkoani Njombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment