Friday, July 11, 2014
MKUTANO MKUU WA BARAZA LA MADIWANI WILAYA YA NJOMBE LA HITIMISHWA JANA
MHANDIS WA UJENZI WILAYA YA NJOMBE
MKURUGENZI HALMSHAURI YA WILAYA YA NJOMBE PAUL MALALA AKIJIBU MASWALI YA WAJUMBE WA BARAZA HILO
Mkutano mkuu wa baraza la madiwani umetaka wawekezaji mbalimbali Wilayani Njombe kusaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka ikiwemo miundombinu ya barabara,zahanati na huduma nyingine kama ahadi za wawekezaji walizotoa wakati wa kusajiliwa.
Kauli hiyo imetolewa na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la madiwani wilaya ya Njombe kufuatia kuwepo kwa baadhi ya wawekezaji kushindwa kutekeleza ahadi zake ambazo huahidiwa wakati wanakaribishwa kuwekeza eneo husika ambapo wametolea mfano wananchi wa vijiji vya Lupembe kushindwa kusafirisha mazao mbalimbali ikiwemo chai na mazao mengine ikiwa wawekezaji wa kiwanda cha chai Ikanga wapo wanasubiri serikali itengeneze.
Miongoni mwa wawekezaji waliolalamikiwa kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuboresha huduma kwa wananchi ni pamoja na kampuni ya kiwanda cha Ikanga ambao waliahidi kujenga mawodi ya kituo cha afya Lupembe,Zahanati ya Kijiji cha Wangingyi na kutengeneza miundombinu ya barabara katika maeneo ya wananchi yanayozunguka maeneo ya uwekezaji lakini hadi sasa wamiliki wa kiwanda hicho hawajafanya hivyo.
Akijibu maswali ya wajumbe wa baraza hilo mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Njombe Paul Malala amesema kuwa halmashauri inatarajia kumuita muwekezaji wa kiwanda cha chai Ikanga kwenye balaza la madiwani litakalo fanyika mwezi augost mwaka huu ili wajumbe waweze kujua uwepo wa kampuni hiyo huku mhandis wa ujenzi wa halmashauri hiyo akisema serikali pia itaingiza kwenye bajeti ya mwaka 2014/2015 na kuweka fedha ya dharula.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Valence Kabelege akifunga mkutano huo amesema kuwa maazimio yote yaliazimiwa na wajumbe wa mkutano huo yanatakiwa kutekelezwa huku akisema kuwa kila mjumbe ameonekana kulalamikia fedha iliyotolewa kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya kila kata kwamba hazikidhi malengo yaliokusudiwa na kwamba hali hiyo inatokana na udhaifu wa ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Amesema kuwa kulingana na bajeti iliyokuwepo kuwa ndogo imesababisha kila kata kupata fedha isiyokidhi matakwa ya miradi iliyoibuliwa ambapo amesisitiza kuwepo kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yataisaidia halmashauri kujiendesha yenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment