Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Sunday, July 13, 2014

KWAYA YA MT. JOSEPH LEO IMEKABIDHI MSAADA WA MASHUKA NA MABLANKETI SABINI KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA NJOMBE-KIBENA

 




 KWAYA YA MT.JOSEPH IKIWA KWENYE WODI LA AKINA MAMA WALIOJIFUNGUA







 MWENYEKITI WA KWAYA YA MT.JOSEPH  BWANA MARIO LUGENGE  AKIZUNGUMZA KABLA YA KUKABIDHI MSAADA HUO.


 MLEZI WA KWAYA  HIYO BWANA EDWARD FRANCIS MWALONGO AKIZUNGUMZA WAKATI WA KUKABIDHI MSAADA HUO.


 MAKABIDHIANO HAPA YANAENDELEA KUFANYIKA


 MGENI RASMI AKIMFUNIKA MAMA NA MTOTO WAKE AMBAE AMETOKA KUJIFUNGUA

 KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA NJOMBE BWANA HAMISI H. CHINDUL AKIZUNGUMZA BAADA YA KUPOKEA MSAADA HUO






 kwaya ya St.Joseph hapa inaimba wimbo wa shukrani wakiwa katika wodi  la akina mama waliotoka kujifungua kibena


 HUYU NI MGANGA MKUU WA HOSPITALI HIYO  DR.JAMES LIGWA





Siku chache baada ya shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Njombe NSSF

Kukabidhi msaada wa taa mbili kwaajili ya chumba cha upasuaji katika hospitali ya Kibena

wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 11,kwa mara nyingine tena Mkuu wa mkoa wa

Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi amepokea msaada wa mashuka na mablanketi sabi

wenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni mbili.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo mwenyekiti wa kwaya ya St.Joseph ya

kanisa Katholiki Jimbo la Njombe bwana Mario Lugenge amesema kuwa  msaada huo ni

mwendelezo wa kanisa Katholiki kupitia kwaya  mbalimbali za kanisa hilo kukabidhi

misaada kwa watu wasiyojiweza,yatima na wagonjwa  kama maandiko ya biblia

yanavyosema.

Aidha bwana Lugenge amesema kuwa kufanikisha zoezi hilo kumetokana na mapato ya

mkanda a Vedeo ambao walitengeneza pamoja na kupata michango kutoka kwa wadau

mbalimbali wa mkoa wa Njombe ambao waliichangia kwaya hiyo na kufanikisha kununua

mashuka 35 na mablanketi 35 ambayo ni mazito kulingana na baridi ya msimu huu.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi

mara baada ya kupokea msaada huyo ,Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Njombe bwana

Hamisi Chindul ameshukuru kwa hatua hiyo na kuwaomba wanakwaya hao kuendelea na

moyo wa kuwasaidia wasiyojiweza huku  taasisi nyingine zikipaswa kuiga mfano huo

kuwasaidia  wagonjwa na vifaa vya hospitali hiyo.

Bwana Chindul amewataka wauguzi  wa hospitali hiyo kuvitunza vifaa mbalimbali

ambavyo  vimekuwa  vikitolewa  na watu wenye mapenzi mema kama msaada kwa

wagonjwa na marekebisho ya hospitali  ili mashirika na watu wenye moyo wa kusaidia 

hospitali hiyo wasikatishwe tamaa na utunzaji na matumizi ya vifaa hivyo.


Kwa upande wake Mganga mkuu wa Hospitali ya Kibena Dr James Ligwa akizungumza

kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe amepongeza kwa hatua hiyo

ya kwaya ya St. Joseph kukabidhi msaada huo na kwamba atahakikisha vifaa hivyo

vinatumika kwa malengo yaliokusudiwa na kuvitunza  visiharibike. 

Hospitali ya mkoa wa Njombe  ya Kibena  imekuwa ikijipatia misaada mbalimbali kutoka

kwa mashirika,taasisi na watu binafsi tangu ilipokabidhiwa kuwa ya mkoa ambapo siku

chache zilizopita shirika la Hifadhi ya Jamii mkoa wa Njombe NSSF na makanisa mjini

Njombe yameanza kupeleka misaada hiyo ili kuboresha mazingira yake na kuwasaidia

wagonjwa baadhi ya huduma.
 


No comments:

Post a Comment