WANACHAMA WA BENKI HIYO WAKIWA KATIKA KUMSHANGIRIA NAIBU WAZIRI WAKATI AKISIMAMA KUTOA HOTUBA YAKE
WANACHAMA WA BENK YA WANAWAKE WAKIWA KATIKA UFUNGUZI HUO
MBUNGE WA NJOMBE KASKAZINI DEO SANGA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WA BENK HIYO NA KUMSHUKURU MKURUGENZI WA BENK HIYO KWA KUSOGEZA HUDUMA HIYO MAKAMBAKO.
MKURUGENZI WA BENK YA WANAWAKE AKIMKARIBISHA NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE JINSIA NA WATOTO DKT PIND HAZARA CHANA
MKURUGENZI WA BENK YA WANAWAKE TANZANIA BI.MAGRATE CHACHA AKITOA TAARIFA FUPI YA MAENDELEO YA BENK HIYO
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII,WANAWAKE,JINSIA NA WATOTO DKT PIND HAZARA CHANA AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANACHAMA WA BENK YA WANAWAKE MJINI MAKAMBAKO
CHEREKOCHEREKO BAADA YA UFUNGUZI WA TAWI KUMALIZIKA
KWA MAKINI KABISA WAKINA MAMA WAKISIKILIZA HOTUBA YA MGENI RASMI
Naibu waziri wa maendeleo ya Jamii, wanawake,Jinsia na Watoto Dkt Pindi Hazara Chana amezindua Kituo cha benki ya wanawake katika halmashauri ya Makambako mkoani Njombe ambapo pamoja na mambo mengine amewataka wananchi kujiunga na Benki hiyo pasipo kujali jinsia.
Akizungumza na wanachama wa Benki ya wanawake wa kutoka Wilaya ya Wanging'ombe,halmashauri ya mji Na Wilaya ya Njombe na Makambako Dtk Pindi Chana amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuzitumia fursa mbalimbali ikiwemo kujiunga na benki zenye masharti nafuu ambazo zitawasaidia akina mama na wananchi wengine wenye kipato cha chini.
Aidha Naibu waziri Chana amemuomba mkurugenzi wa Benki ya wanawake Bi.Magreth Chacha kusogeza huduma hiyo ya benki ya wanawake katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Njombe ikiwemo Wilaya ya Wanging'ombe,Njombe,Ludewa na Makete huku akiwataka wanachama wa benki hiyo kuzingatia masharti ya mikopo kwa kutokiuka urejesha wa mikopo hiyo na kwamba serikali itahakikisha inashirikiana kikamilifu ili kupambana na wimbi la umasikini.
Amesema kuwa viongozi wa benki hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji na mitaa pamoja na wanachama wawafikie wananchi wengine kutoa elimu ya kujiunga na benki hiyo huku wakitakiwa kuwa makini katika suala la kurejesha mikopo ili kukuza huduma hiyo ya benki ya wanawake mkoa wa Njombe.
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya Benki ya wanawake Mkurugenzi wa Benki hiyo Tanzania bi. Magreth Chacha amesema kuwa Benki ya wanawake ilianza mwaka 2009 kwa kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa lengo la kuwainua wanawake kiuchumi ambapo ilianza na mtaji wa shilingi milioni mbili nukta nane na kufikia shilingi bilioni mbili nukta tatu ambayo ipo kwa sasa na kusema kuwa ufunguzi wa benki hiyo ni ukombozi kwa wanawake.
Kwa upande wao wanachama wa benk hiyo ambao wameshiriki wakati wa uzinduzi wa kituo cha Benki hiyo mjini Makambako wameshukuru serikali kwa kuunga mkono kuanzishwa kwa benk hiyo na kwamba itawasaidia katika kukabiliana na wimbi la umasikini kwani mwananchi anaruhusiwa kujiunga hata kama anashiringi elfu tatu.
No comments:
Post a Comment