Polisi Wakiwa Eneo la Tukio Mapema Leo
Katikati n mlinzi
aliyejaribu kupambana na majambazi hao hadi kuchaniwa Suruali ya Kazi
lakini wakafanikiwa kutokamea kusiko julikana
MASHUHUDA WAKIANGALIA MWILI WA MLINZI HUYO ALIYEUWAWA NA MAJAMBAZI HAO.
Mwili wa marehemu adamu kiswaga aliyeuwa katika lindo ukipelekwa hospitali
Hii ni taswira ya Mji wa Njombe Ambako Matukio ya Mauaji Yamekuwa Yakijitokeza MAUAJI HAYA YANAYOWAKUTA WALINZI MJINI NJOMBE YAMEKUWA NI YA MUENDELEZO SASA KUMBUKA MWAKA 2013 MLINZI MMOJA WA STATIONARY YA MAYEMBA NYUMA YA KANISA LA ROMAN KATHOLIKI MJINI NJOMBE ALIKUTWA AMEUWAWA NA MAJAMBAZI,MWAKA HUU WA 2014 MLINZI WA MADUKA MTAA WA RAMADHANI MJINI NJOMBE AMEUWAWA NA MAJAMBAZI NA LEO HII AMEKUTWA MLINZI MJINI HAPA AKIWA AMEUWAWA NA MAJAMBAZI AMBAO HAWAJAPATIKANA WALIKOELEKEA.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mlinzi wa Maduka Matatu Mjini Njombe Adamu Kiswaga Mwenye Umri Kati ya Miaka 45-50
Ameuawa na Watu Wasiofahamika Usiku wa Kuamkia jana akiwa katika eneo lake la kazi
Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nane Usiku Katika Eneo la Nyumba ya Kulala Wageni ya
Amani Lodge Mkabala na Kituo Cha Mafuta Cha GAPCO Ambapo Mlinzi Huyo Ameuawa na Kitu
Kizito Kichwani Wakati Akiwa Lindoni.
Wakizungumza na www.gabrielkimlya.blogspot,.com Baadhi ya Mashuhuda na Walinzi Waliokuwepo Katika Eneo la
Tukio Wamesema Kuwa Mlinzi Huyo Ameuawa na Watu Wawili Ambao Hawakuweza
Kuwatambua Wakati Wakitaka Kujaribu Kubomoa Nyuma ya duka la Mzee Makete Kwa Lengo
Aidha Baada ya Kumuuwa Mlinzi Huyo Ndipo Walipotaka Kuanza Kubomoa Jengo Hilo na Kisha
Kukutana na Walinzi Toka Maeneo Mengine na Waka pambana Nao Pasipo Silaha za Moto Kisha
Watu Hao Wanaodhaniwa Kuwa ni Majambazi Wakapata Mwanya wa Kutoroka.
Baadhi ya Wahudumu na Wateja Waliolala Katika Nyumba Hiyo ya Amani Lodge Wamesema
Kuwa Mara Nyingi Walinzi Katika Eneo Hilo Wamekuwa Wakiota Moto Nyuma ya Nyumba Hiyo
Katika Jiko la Kuchemshia Maji huku wakiacha malindo yao bila ulinzi.
Rodgers Mhagama ni Mmoja wa Waajiri wa Mlinzi Huyo Katika Maduka Hayo Ambaye Amesema
Kuwa Mlinzi Huyo Alikuwa Akilinda Kwa Kutumia Silaha za Jadi Hali Iliyosababisha Mlinzi Huyo
Kuzidiwa Nguvu.
Hadi kamera ya mtandao huu Ikiondoka Katika Eneo la Tukio Jeshi la Polisi Lilikuwa Limefika na Kuchukua Mwili wa Marehemu Huyo.
No comments:
Post a Comment