MKURUGENZI WA VETA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI BI.MONICA MBELLE
MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE WA MWISHO KUSHOTO VALENCE KABELEGE NA WA PILI TOKA KUSHOTO MKURUGENZI MAMLAKA YA MAJI MJINI NJOMBE BWANA MAJANI
MGENI RASMI AFISA ELIMU MKOA WA NJOMBE SAID NYASIRO AKITOA HOTUBA YAKE MAPEMA LEO
MWENYEKITI WA BOD YA YETA KANDA YA NYANDA ZA JUU KABAKA S.NDENDA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUZUNGUMZA NA WADAU WA MAENDELEO
WADAU WA MAENDELEO MKOA WA NJOMBE WAKIENDELEA KUBADILISHANA MAWAZO JUU YA KUIMARISHA NA KUHAMASISHA VIJANA KUJIAJIRI BAADA YA KUPATA ELIMU YA UFUNDI STADI
PICHA YA PAMOJA NA MGENI RASMI WAKIWA KWENYE SEMINA YA SIKU MOJA MAPEMA LEO
SEMINA BADO INAENDELEA KATIKA UKUMBI WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI NJOMBE NA HUYU NI MKURUGENZI WA VETA NYANDA ZA JUU KUSINI AKITOA MADA
Serikali inatarajia kujenga vyuo vya Ufundi Stadi vya VETA kwa halmashauri za Ludewa, Makete na kuvijengea uwezo vyuo vya Ulembwe Wilayani Wanging'ombe na Chuo cha maendeleo ya wananchi Mjini Njombe pamoja na kujenga chuo cha Ufundi Stadi VETA Mkoa kitakachojengwa makao makuu yaliyopo halmashauri ya mji Njombe.
Akiongea na Watumishi na wadau wa Maendeleo kwenye semina ya siku moja kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptain Mstaafu Aseri Msangi,Afisa Elimu mkoa wa Njombe Said Nyasiro amesema mkoa wa Njombe unavyuo vya ufundi mbalimbali vya serikali na watu binafsi ambavyo vilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu ya ufundi stadi kwa vijana ili waweze kujiajiri wenyewe.
Aidha Bwana Nyasiro amesema serikali imetenga fedha kwaajili ya kujenga chuo cha Ufundi Stadi Veta cha mkoa kitakachojengwa halmashauri ya mji wa Njombe Eneo la Magoda na kusema inakabiliwa na tatizo la kukosekana kwa fedha za kuwalipa fidia wananchi waliopo eneo lililopendekezwa kujengwa chuo hicho jambo ambalo limesababisha kushindwa kuanza Ujenzi huo.
Bwana Nyasiro amesema mwaka 2013 wanafunzi waliohitimu elimu ya darasa la saba walikuwa elfu 19 na 30 na waliokwenda kujiunga na masomo ya sekondari walikuwa takribani elfu tisa kwa mkoa na waliofanikiwa kujiunga na kidato cha tano hawakuzidi elfu moja kati ya wanafunzi elfu 12 wa sekondari na waliosalia wanahitaji kujiajiri na kuajiliwa katika taasisi za serikali na binafsi. na kwamba sehemu kuu ya ajira ni sekta ya ufundi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Vyuo vya Ufundi Stadi VETA Nyanda za juu kusini bwana Kabaka Ndenda amewataka wadau wa maendeleo kuyatumia mawazo wanayopata kwenye semina hiyo iliowakutanisha viongozi wa VETA na kujadili mambo mbalimbali yanayohusu mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi na kuboresha sekta hiyo ambapo wananchi wanatakiwa kutambua umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo ili kupata ujuzi na soko la ajira kwa Vijana.
Awali Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Nyanda za Juu kusini Bi.Monica Mbelle Akizungumza mbele ya Mgeni Rasmi amesema Ufundi Stadi ni Silaha dhidi ya kupambana na Adui Umasikini na kwamba jamii ikizingatia uwepo wa mafunzo ya ufundi stadi itasaidia kupunguza tatizo la Ajira.
Bi.Mbelle amewataka wadau wa maendeleo kuwaelimisha vijana kujiunga na mafunzo ya Ufundi Stadi wakati serikali mkoa wa Njombe ikiendelea kujenga vyuo vya Ufundi stadi vya Ludewa na Chuo cha VETA Mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na Vyuo vya watu binafsi elimu hiyo itaboreshwa kwa nchi Nzima Ambapo lengo la Warsha hiyo ni kutoa elimu kwa wadau kuhusiana na ufundi stadi.
Semina hiyo imelenga kuwahamasisha wadau wa Mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma kwa lengo la kuwakutanisha na kukumbushana juu ya kuhamasisha vijana na wazazi kupeleka watoto wao kupatiwa mafunzo ya ufundi stadi kwa manufaa yao ya baadae na taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye ziara hapo mwaka jana 2013 akiwa Wilaya ya Ludewa alisema serikali inatarajia kujenga Vyuo vya Veta kwa Mkoa wa Njombe na chuo cha ufundi stadi Ludewa kitakachojengwa Kijiji cha Shauri Moya kata ya Mundindi pamoja na kuagiza wazazi kupeleka watoto kujifunza mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment