Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, May 16, 2014

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE SARAH DUMBA AHIMIZA ELIMU YA MASHAMBA DARASA IENEE KOTE KWA WANANCHI

mgeni rasmi akielekea kukagua shamba la waliopatiwa mafunzo ya shamba darasa matiganjora
























 MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA KATIKA KIJIJI CHA MATIGANJORA WILAYANI NJOMBE  AKITOA HOTUBA YAKE KWA WANANCHI

Mkuu wa Wilaya ya Njombe amewapongeza wananchi wa kijiji cha Matiganjora Wilayani Njombe kwa kujiunga katika kikundi cha shamba darasa na kujituma kufanya shughuli za kilimo ambapo amewataka kuwa wavumilivu na changamoto zinazowakabili  na kuwataka kutambua kuwa penye changamoto pana fursa mbalimbali za maendeleo kwaajili yao.

Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho mwishoni mwa wiki iliyopita Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Dumba amewataka wakulima na viongozi wa vijiji na kata ya Ikuna kuongeza ubunifu katika kilimo cha mashamba darasa kupitia mafunzo waliopatiwa na shirika la NADO ili waweze kupata mafanikio makubwa.

Aidha Bi.Dumba amesema kuwa viongozi na wananchi wanatakiwa kudumisha umoja na mshikamano katika kufanya kazi ikiwemo kuanzisha mashamba ya kilimo cha nyanya,viazi pamoja na kujiunga katika vikundi vya Benki za wananchi Vijijini VIKOBA kwa manufaa yao na kwaamba Vikoba ni mfumo wa kifedha utakaowasaidi kutatua baadhi ya changamoto zikiwemo za kilimo.

Amesema kuwa wakulima wanatakiwa kuwashirikisha wataalamu wa kilimo na Mifugo katika shughuli zao zinazofanyika za kilimo na ufugaji  na kuwataka wazingatie kwa dhati maelezo yanayotolewa na wataalamu ili kupata kipato cha kutosha na kukidhi mahitaji yao ya kifamilia.

Akisoma Risala fupi kwa Mgeni rasmi kwa niaba ya wanakikundi cha Shamba darasa cha Mshikamano cha Matiganjora bi.Grace Nyagawa amesema kuwa kikundi hicho kina jumla ya wanachama hamsini ambao wamepatiwa mafunzo hayo na shirika la NADO na ADA kwaajili ya kilimo cha nyanya na Viazi ambapo ameeleza kuwa wakulima wanakabiliwa na ugonjwa unaoshambulia  mazao hayo.

Aidha amesema kuwa kikundi hicho kinakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa mtaji  kwaajili ya kuendeshea shughuli zao za kijasiliamali na kilimo ambapo kina mikakati  ya kujiunga na Benki za wananchi Vijijini VIKOBA na kwamba hadi sasa kimefeli kiasi cha fedha cha shilingi laki mbili na na hamsini kwani kina shilingi elfu hamsini tu.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo ya shamba darasa ambayo yametolewa na shirika la NADO kijijini humo wameshukuru kwa kupewa elimu hiyo ambapo wamesema kuwa mpaka sasa kila mkulima ameanza kulima kwa kutumia elimu  ya kilimo cha shamba darasa ambayo walipewa mwezi uliopita

No comments:

Post a Comment