Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, May 7, 2014

MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA ATAKA KUZOLEWA KWA TAKA WILAYANI HUMO



 HIZI NI TAKA AMBAZO HAZIJAZOLEWA KUTOKANA NA WANANCHI KUKATAA KUCHANGIA MCHANGO WA SHIRINGI ELFU TATU KWA MADAI HAWAKUSHIRIKISHWA WAKATI WANAPITISHA SHERIA YA MCHANGO HUO BADALA SHILINGI ELFU MOJA AMBAYO WALIKUWA WAKIICHANGIA HAPO AWALI,WANADAI HALMASHAURI ZIMEPITISHA PASIPO WAO KUSHIRIKISHWA WANASHANGAA WANADAIWA HELA HIYO TU.





 SHIDA YOTE YA WANANCHI KUTOCHANGIA SHILINGI ELFU TATU NI KWAMBA HAWAKUSHIRIKISHWA AWALI WALIKUWA WAKITOZWA ELFU MOJA KWA KILA NYUMBA LEO WANATOZWA ELFU TATU KWA KILA NYUMBA WANAHOJI SHERIA IMEPITISHWA NA NANI MBONA WAO HAWAJASHILIKISHWA KAMA WANARIDHIA KUPITISHWA KWA PESA HIYO?


Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sarah Dumba amezikumbusha halmashauri za mji wa Njombe na Makambako kuhakikisha zinatekeleza jukumu la kuondoa taka kwenye vizimba vya taka hizo  ambapo pamoja na mambo mengine wananchi nao wameombwa kushiriki uchangiaji fedha kwaajili ya kusaidia kuondoa uchafu huo.

Akizungumza na Uplands fm radio Mkuu wa Wilaya ya Njombe bi.Sarah Dumba amesema kuwa ili halmashauri iweze kupatiwa hati safi ya usafi wa mazingira wananchi kwa kushirikiana na viongozi wa mitaa na vijiji wanatakiwa kutambua umuhimu wa kuchangia kuliko kuiachia halmashauri pekee jambo ambalo hazitaweza kumudu uzoaji wa taka hizo.

Aidha Bi.Dumba amesema kuwa kutokana na ongezeko la wakazi wa halmashauri za mji wa Njombe na Makambako uzalishaji wa taka umekuwa ukiongezeka siku hadi siku tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo jitihada mbalimbali zinatakiwa kufanyika katika kuhakikisha usafi wa mazingira unakuwepo ili kuepukana na milipuko ya magonjwa.

Kauli hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Dumba imekuja kufuatia kuwepo kwa takataka nyingi kwenye vizimba mbalimbali Mjini Njombe na Makambako jambo linalotishia usalama wa afya za wakazi wa maeneo hayo ambapo amesema cha kushangaza zaidi baadhi ya wananchi wanatupa uchafu huo  kwenye vyanzo vya maji.

Halmashauri za mji wa Njombe na makambako tayari zimekwisha kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa halmashauri ya mji wa Makambako imekwisha pata gari la kuzolea taka hizo huku halmashauri ya mji wa Njombe ikiwa na magari mawili kwaajili ya kuzolea taka hizo na kuweka miji katika hali ya usafi.





No comments:

Post a Comment