|
Kutoka
kushoto mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madah ,mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazani Zitto
Kabwe wakiwa katika msiba wa babake Filikunjombe mjini Ludewa mchana wa
leo |
|
Naibu
waziri wa maendeleo ya wanawake na watoto Pindi Chana na mkuu wa
wilaya ya Njombe Sarah Dumba kulia kushoto ni mwenyekiti wa CCM Ludewa
Bw Stanley Kolimba |
|
Mbunge Filikunjombe kushoto akifarijiwa |
|
Katibu
wa itikadi na uenezi mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya akimwomba Zitto
Kabwe kusaidia kushirikiana na mbunge Filikunjombe juu ya ubovu wa
miundo mbinu Njombe- Ludewa |
|
Kamanda wa polisi Njombe |
|
DC Ludewa Bw Juma Madaha akitambulisha viongozi mbali mbali |
|
Mbunge
Zitto Kabwe kulia akimfariji mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe leo
mjini Ludewa kwa kifo cha babake mbunge Filikunjombe |
|
Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwa na mbunge Zitto Kabwe kulia |
|
Timu ya wabunge waliofika kumfariji Filikunjombe leo |
|
Mbunge Zitto Kabwe kushoto akishiriki msosi na mbunge Deo Filikunjombe |
|
Mbunge Filikunjombe kulia akiteta jambo na mdogo wake Philipo ambae alikuwa akimuuguza babake Dubai na India |
|
RPC Njombe akiongoza msafara wa mazishi hayo hii ni polisi jamii ulinzi shirikishi |
|
Mbunge wa jimbo la Mwibara Kang Lugola akishuka katika gari |
|
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akilitazama jeneza lenye
mwili wa babake marehemu Frolian Filikunjombe likiingizwa ndani ya
kanisa la RC Ludewa kwa ajili ya ibada ya mwisho kabla ya mazishi
yaliyofanyika katika makaburi ya Ludewa mjini |
MBUNGE
wa jimbo la Kigoma Kasikazin Zitto (CHADEMleo amegeuka kuwa
kivutio kikubwa katika mazishi ya babake mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe huku wananchi wa jimbo hilo na viongozi wa CCM mkoa
wa Njombe wakimbebesha
majukumu ya ubovu wa barabara kwa kumtaka kushirikiana na mbunge
wao kuwasha moto bungeni .
Zitto
ambae katika msafara wake huo aliongozana na mbunge wa jimbo la
Mwibara Kangi Lugola (CCM) mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Amina
Mwidau (CUF) na wengine wa CCM nusuru avuruge msiba huo baada ya
wananchi kuonyesha kuvutiwa na uwepo wake na kumtaka kusikia
sauti yake .
Awali
wakati wa utambulisho wa viongozi wa kitaifa uliofanywa na mkuu wa
wilaya ya Ludewa Juma Madaha waombolezaji baada ya kusikia jina la
Zitto Kabwe katika orodha ya wabunge hao ndipo sauti ziliposikika
kuwa wanahitaji azungumze .
Hata
hivyo katika salam zake katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa
Njombe Honoratus Mgaya mbali ya kumpongeza mbunge Kabwe kwa kufika
katika msiba huo na timu yake bado alimtaka Kabwe na timu yake
kusaidiana na mbunge wao Filikunjombe kupigania ujenzi wa barabara ya
lami kati ya Ludewa na Njombe.
"Mheshimiwa
Zitto Kabwe wewe ni mmoja kati ya wapiganaji wa kweli bungeni kama
alivyo mbunge wetu na jembe letu wana Ludewa Deo Filikunjombe
....sasa tunaamini mmeona ubovu wa barabara ya Njombe - Ludewa hivyo
kupitia ninyi sisi wana Njombe na Ludewa tunaomba msaidiane na
Filikunjombe kupigania suala la ubovu wa barabara na sio kutoka nje ya
bunge pindi suala la ubovu wa miundo mbinu linapotolewa na mbunge
wetu"
Kufuatia
ombi hilo la Mgaya waombolezaji walilipuka kwa furaha huku Zitto
Kabwe akionyesha kuguswa na ombi hilo na kumtania mbunge wa viti
maalum mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF) kuwa UKAWA hao .
Zitto
Kabwe ambae alikuwa ni mmoja wa abiria waliosafiri pamoja na babake
Filikunjombe mzee Frolian Filikunjombe kabla ya kufariki dunia akiwa
ndani ya ndege kutoka Dubai kuja nchini ni mmoja wa marafiki
wakubwa wa mbunge Filikunjombe na pia ni mwenyekiti wa kamati ya PAC
ambapo Filikunjombe ni makamu mwenyekiti wake.
Hata
hivyo
alisema kuwa ombi la wana Ludewa kwake atalifanyia kazi na kuwa
suala la siasa lina sehemu yake na yanapozungumzwa mambo ya kimaendeleo
siasa za vyama zinawekwa kando .
Hivyo
alisema kuwa kutokana na mahusiano mema kati yake ya mbunge
Filikunjombe ameguswa na msiba huo na kuwa pindi atakapofika bungeni
maombi ya wana Ludewa atayatendea kazi
.
KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN
No comments:
Post a Comment