Haya ni Maandamano Ya Baadhi ya Wafanyakazi Wakiingia Katika Viwanja wa Sabasaba Mjini Njombe,MEI MOSI
tEaM uPlAnDs
Vijana Wapiga Kazi UPLANDS FM Wakijiandaa Kurusha Matangazo Ya Moja Kwa Moja Wakati wa Sherehe Ya Mei Mosi Njombe Leo.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akihutubia Wafanyakazi Kwenye Mei Mosi Leo Njombe
Mkuu
wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akizungumza na Mamia Ya Wafanyakazi
Mkoani Njombe Kushoto Kwake ni Br.Novatus Lyaruu Toka Uplands Fm Radio
Akirusha Matangazo Ya Moja Kwa Moja
Team Uplands fm wakiwa Katika Viwanja Vya Sabasaba Njombe leo Mei Mosi.
Na Michael Ngilangwa Njombe
Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu Aseri Msangi Amewataka Waajiri wa
Serikali na Sekta Binafsi Kuwaruhusu Wafanyakazi Wao Kuanzisha Mabaraza
ya Wafanyakazi Kazi Pamoja na Kujiunga Kwenye Vyama Vya Wafanyakazi .
Akiongea
Kwenye Sherehe za Mei Mosi Kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya
Njombe Bi. Sara Dumba Ambaye Alikuwa Mgeni Rasmi Amesema ni Haki ya
Kikatiba Kwa Mfanyakazi Kujiunga na Chama cha Wafanyakazi, Hivyo Waajiri
Hawatakiwi Kuwazuia Wafanyakazi Wao Kujiunga na Vyama Hivyo.
Adhia
Bi. Dumba Amewataka Waajiri Kufanya Vikao Vya Mara Kwa Mara na
Wafanyakazi Ama Viongozi wa Vyama Vya Wafanyakazi Ili Kupunguza
Migogoro na Kero Zinazowakabili Sehemu Zao za Kazi, Huku Akiwaagiza
Waajiri wa Serikali na Sekta Binafsi Kuhakikisha Wanalipa Madai Yote ya
Wafanyakazi Wao
Akizunguzia Suala la Mapendekezo ya Mshahara Kwa
Kima cha Chini Kianzie 315,000 Kilichopendekezwa na Shirikisho la Vyama
Vya Wafanyakazi Nchini TUCTA , Bi Dumba Amesema Amepokea Mapendekezo
Hayo na Kulifikisha Katika Ngazi Husika Ili Lipatiwae Ufumbuzi.
Awali
Akisoma Taarifa Fupi ya Wafanyakazi Mratibu wa Maadhimisho Hayo Mkoani
Njombe Ambae Pia ni Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Mkoa wa Njombe
Bwana Zambi Amesema Wafanyakazi Wanakabiliwa na
Changamoto Kadhaa Ikiwemo Baadhi ya Waajiri Kuwatishia Kuwafukuza Kazi Wafanyakazi Wao Pamoja na Kulipwa Mishahara Midogo
Kwa
Upande Wao Baadhi ya Wafanyakazi Waliopata Vyeti Vya Mfanyakazi Hodari
Wamewashukuru Waajiri Wao Kwa Kuwatunuku Vyeti Pamoja na Zawadi Huku
Wakiwataka Waajiri Ambao Wameshindwa Kutii Agizo la Mkuu wa Mkoa wa
Njombe la Kuwapatia Zawadi Wafanyakazi Wao Waliofanya Vizuri Kutii agizo
hilo.
Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Husherehekea
Kila Tarehe Moja ya Mwezi wa Tano Kila Mwaka Ambapo Kaulimbiu ya Mwaka
Huu ni UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI , Kauli Hiyo
Inawahimiza Watawala Kuwa Bora na Kutatua Kero za Wafanyakazi Wao
Kitaifa
Maadhimisho Hayo Yamefanyika Katika Viwanja Vya Uhuru Jijini Dar Es
Salaam Huku Rais Jakaya Kikwete Akiwa Mgeni Rasmi , na Kwa Mkoa wa
Njombe Yamefanyikia Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe .
No comments:
Post a Comment