Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Akizungumza Kwenye Kikao Cha Baraza la Madiwani.
Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Richard Ngwale Akizungumza Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani.
Baadhi ya Wa Madiwani Katika Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Wakiwa Kwenye Kikao cha Baraza.
Na Gabrie Kilamlya Wanging'ombe
Serikali
Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Imetenga Zaidi Ya Shilingi Milioni
100 Kwa ajili ya Kutekeleza Miradi Mbalimbali Ya Kimaendeleo Ikiwemo
Ununuzi wa Vyombo Vya Usafiri.
Akizungumzia Suala la Bajeti
Iliyotengwa Kwa Ajili ya Kutekeleza Miradi Mbalimbali Mkuu wa Ya
Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Amesema Kuwa Jumla ya Shilingi Milioni
150 Zitatumika Kwa Ajili ya Ununuzi wa Magari Kutokana na Uhaba Mkubwa
wa Vyombo Vya Usafiri Katika Halmashauri Hiyo.
Aidha Bi.Esterina
Kilasi Amewataka Madiwani Kushirikiana na Viongozi wa Ngazi za Vijiji
na Kata Kuhakikisha Wanawasimamia Wakandarasi Wanaotekeleza Miradi
Mbalimbali ya Maendeleo Ndani ya Kata na Vijiji Vyao.
Bi. Kilasi
Ametoa Agizo Hilo Kwenye Kikao cha Baraza la Madini la Halmashauri ya
Wilaya ya Wanging'ombe Wakati Akitoa Salaamu za Serikali Kwa Madiwani
Hao.
Amesema Kuwa Jitihada za Madiwani na Viongozi Mbalimbali
Katika Kusimamia Miradi Hiyo Itasaidia Kufanyika Kwa Kazi Yenye Ubora na
Viwango Ili Kukuza na Kutekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu Ya Mwaka
2010/2015.
Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Amewataka Madiwani Hao
Kuendelea Kuwahamasisha Wananchi Kujenga Nyumba Zenye Uwezo wa Kuingiza
Miundombinu ya Umeme Katika Maeneo Yao Kwani Serikali Itasongeza Huduma
za Umeme Kwenye Vijiji Katika Kipindi cha Fedha cha Mwaka Huu.
No comments:
Post a Comment