Tuesday, May 27, 2014
KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AITEKA HANANG,AIBOMOA NGOME YA CHADEMA MKOANI MANYARA.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndug Kinana akimhoji kwa kifupi Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba (aliyehudhuria mkutano wa hadhara wa chama cha CCM), alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani analipwa na uko wapi..
Hatua hiyo ya kumhoji ilifikiwa baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto, kuwa viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba ili serikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo.
Katibu wa NEC Itakadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Hanang,Bwa.Augustino Mayumba mara baada ya kujibu tuhuma mbele ya Wananchi kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,akidaiwa kuficha mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha hizo haijulikani nani analipw a na uko wapi.
Katibu Mkuu wa CCM,akipeana mkono na Katibu Kata wa CHADEMA,wa Kata ya Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas mara baada ya kukabidhi kadi yake cha chama hicho na kujiunga na chama cha CCM
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na wafuasi wakuu wa CHADEMA,walioamua kujiunga na chama chama CCM baada ya kuzikabidhi kadi zao kwa Ndugu Kinana.Kulia ni Meshack Kim,Katibu Kata wa CHADEMA,waka Kata ya Gendabi,Wilayani Hanang,Bwa,Aman Lucas na mwisho kushoto ni Elisante Taulo.
Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Hanang na Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Frederick Sumaye akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Hanang, Dk. Mary Nagu walipokuwa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Gendabi kata ya Gendabi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye akipokea mabango yenye jumbe mbalimbali yaliokuwa yamebebwa na wananchi,katika mkutano wa hadhara uliofanyika Endasak,Wilayani Hanang mkoani Manyara,pamoja na hayo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alitoa majibu kwa wananchi hao na kuonesha kuridhika nayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment