KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOA WA NJOMBE SACP FULGENCE NGONYANI AKIWA OFISINI KWAKE LEO
Kutokana na Ongezeko la Matukio Hayo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema
Halitasita Kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria Wale Wote Watakaobainika Kujichulia
Sheria Mkononi Dhidi ya Wahalifu Au Matukio ya Aina Yeyote Katika Jamii.
Rai Hiyo Imekuja Kufuatia Kuwepo Kwa Watu Wanaojichukulia Sheria Mikononi Dhidi ya
Wahalifu Badala ya Kuwafikisha Katika Vyombo Vya Sheria Kuliko Kuchukua Sheria
Mikononi Kwani Kufanya Hivyo ni Kosa La Jinai.
Akizungumza na Uplands Fm Radio Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kamanda
wa Jeshi Hilo Fulgence Ngonyani Amesema Kumekuwepo na Watu Wanaojichukulia
Sheria Mikononi Hivyo Jeshi la Polisi Litahakikisha Linawakamata na Kuwafikisha Katika
Vyombo Vya Sheria Ili Kuwa Fundisho Kwa Wengine.
Kamanda Ngonyani Amewataka Wananchi Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi la Polisi Katika
Kuwafichua Wahalifu Kwenye Jamii Ambapo Amesema Kwa Ushirikiano Huo Suala la
Uhalifu Linaweza Kupungua Endapo Ushirikiano Utatolewa.
Suala la Kuchukua Sheria Mkononi ni Kosa la Jinai Hivyo Wananchi Wanawajibu wa
Kutambua Kuwa Sheria Ndiyo Chombo Cha Usuluhishi Huku Ushirikiano Kwa Jeshi la
Polisi Ukipewa Kipaumbele Kufichua Uhalifu Mjini Njombe.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo linawashikilia watu wawili Sharif Mhagama na Ally
Mlelwa kwa tuhuma za kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kinyume na sheria.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani amesema kuwa
watuhumiwa hao Sharifu Mhagama na Ally Mlelwa walikamatwa na dawa hizo baada ya
msako mkali uliofanywa na kikosi cha jeshi la polisi mnamo mei 27 majira ya saa moja na
nusu jioni wakiwa mtaa wa Chaugingi
No comments:
Post a Comment