AFISA USALAAMA WA TAIFA WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE BWANA ISSAYA MOSES AKIWAASA WATUMISHI HAO KABLA HAWAJARUHUSIWA KWENDA KUANZA KAZI RASMI KATIKA MAENEO YAO.
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKITOA HOTUBA YAKE KWA WATUMISHI WAPYA WALIOPATA AJIRA MWAKA HUU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
MGENI RASMI MKUU WA WILAYA YA NJOMBE AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA WATUMISHI WAPYA WALIOPATA AJIRA MWAKA HUU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Amewaasa Watumishi Waliopata Ajira Mpya Wilayani Humo Kufanyakazi Kwa Kuzingatia Sheria na Maadili ya Kazi Zao , Ambapo Pia Amewataka Kujiepusha na Migogoro Isiyo ya Lazima na Waajiri Wao Mahala Pa Kazi .
Akizungumza Wakati wa Akifungua Semina ya Siku Mbili Kwa Watumishi Hao Wapya Inayolenga Kuwakumbusha Maadili ya Kazi Ikiwemo Kutunza Siri za Ofisi, Bi. Dumba Amewataka Watumishi Hao Kudai Haki Zao Kwa Njia ya Mazungumzo Badala ya Kufanya Maandano Ambayo Huleta Migogoro Mahala Pa Kazi .
Aidha Bi.Dumba Pia Amewataka Watumishia Hao Kuwajibika Kikamilifu Kwa Waajiri Wao na Kujiepusha na Masuala ya Itikadi za Kisiasa Mahala Pa Kazi na Kujihadhari na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi ,Kama Anavyoeleza.
Awali Akizungumza Wakati Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Issaya Moses Amewataka Watumishi Hao Kuheshimu Nafasi za Kazi Walizozipata na Wasiwe Chanzo cha Matatizo na Kusababisha Vurugu Mahala Pa Kazi , na Hapa Anaeleza.
Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Msena Bina Amesema Jumla ya Watumishi 162 Wapya wa Sekta za Elimu na Afya Wameshiriki Katika Semina Hiyo Ambayo Inalenga Kuwaongezea Uwezo wa Kuyafahamu Majukumu Yao na Kuzingatia Sheria za Ajira na Mahusiano Kazini .
No comments:
Post a Comment