Tuesday, May 13, 2014
CHADEMA WAFUNGUA TAWI MTAA WA MATALAWE MJINI NJOMBE
DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGRY MTAMBO AKIFUNGUA TAWI LA CHADEMA MTAA WA MATALAWE
ABU MTAMIKE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI MATALAWE
KAIMU KATIBU WA CHADEMA WILAYA YA NJOMBE ALATANGA NYAGAWA AKIZUNGUMZA NA WANACHAMA WAKE
WANANCHI WA MTAA WA MATALAWE WAKISIKILIZA HOJA ZA VIONGOZI WA CHADEMA WAKATI WA UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA TAWI LA MATALAWE
`Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mjini Njombe Kimewataka Vijana Kuacha Tabia ya Kukaa Vilingeni Pasipo Shughuli Yoyote na Badala Yake Wazitumia Fursa Zilizoko Katika Maeneo Yao Kwa Ajili ya Kujikwamua Kiuchumi.
Rai Hiyo Imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema BAVICHA Kata ya Njombe Mjini Hashimu Mkane Wakati wa Ufunguzi wa Ofisi ya Tawi la Chama Hicho Katika Mitaa ya Matalawe na Buguruni Mjini Njombe, na Kuwashauri Vijana Kuachana na Tabia ya Kusubiri Ajira Kutoka Serikalini.
Aidha Bwana Mkane Amewashauri Vijana Kujiunga Kwenye Vikundi Vya Mbalimbali na Kuanzisha Shughuli za Ujasiliamali na Kuacha Tabia ya Kuchagua Kazi Kama Wanavyofanya Baadhi ya Vijana .
Naye Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Amewataka Wananchi Kushirikiana na Viongozi Wao Katika Kuleta Maendeleo Kwenye Maeneo Yao , Huku Akikemea Tabia ya Baadhi ya Watumishi Wasiowaadilifu Wanaowadai Wananchi Kwa Ajili ya Kuwawekea Dhamana Ndugu Ama Jamaa Zao Ambao Wanaoshikiwa Kwenye Mabaraza ya Kata Au Kituo cha Polisi .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment