Saturday, March 15, 2014
ZAIDI YA MITI 500 YA MATUNDA ITAPANDWA KWA NYAKATI TOFAUTI
HII NI MITI YA MATUNDA YA SHULE YA MSINGI NYOMBO
HUYU NI MWALIMU MKUU WA SHULE YA MSINGI NYOMBO JOHN LUKOGERA AKIONESHA NAMNA MITI AINA YA PARACHICHI INAVYOWEZA KUZAA MATUNDA NA KWA MUDA MFUPI
HII NI SHULE YA MSINGI NYOMBO
Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Nyombo kata ya Ikuna Wilayani Njombe bwana John Lukogera amesema kuwa shule hiyo inatarajia kupanda zaidi ya miti hamsini ya matunda aina ya parachichi kwaajili ya kuiingizia kipato shule hiyo pamoja na kuwajengea mazoea ya kutumia matunda kwa wanafunzi.
Akiongea na Uplands fm mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyombo bwana Lukogera amesema kuwa shule hiyo Kwa kipindi cha mwaka huu katika wiki la upandaji miti ilifanikiwa kupanda miti mia nane aina ya paine kwaajili ya mbao ikiwa na matarajio ya kufikisha miti mia tano ya matunda ambayo itapandwa kwa awamu tofauti.
Aidha bwana Lukogera amesema kuwa hatua hiyo imekuja kufuatia shule hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali za uchangiaji wa michango kwaajili ya chakula na mahitaji mengine ambapo mradi wa matunda unaweza kusaidia kupunguza michango kwa wazazi na kukuza kipato cha shule hiyo.
Bwana Lukogero amewataka wananchi wa kijiji cha Nyombo kwa kushirikiana na viongozi wao kutoa kipa umbele katika sekta ya upandaji wa miti ya matunda kwa manufaa yao na kuongeza uchumi wa kila mmoja na kwamba matunda mbalimbali ikiwemo maparachichi huanza kuchumwa matunda baada ya miaka miwili na hivyo ni mkombozi kwa uchumi wa jamii.
Serikali mkoani Njombe imekuwa ikihamasisha wananchi kushiriki katika upandaji wa miti mbalimbali ikiwemo ya matunda na miti ambayo ni rafiki kwa vyanzo vya maji pamoja na kutunza mazingira ili kurudisha uoto wa asili uliokuwepo zamani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment