Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Tuesday, March 18, 2014

WAWILI WASHIKILIA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

 
KAMANDA WA JESHI LA POLISI  MKOA WA NJOMBE FULGENCE NGONYANI

ASP Florence Ibrahim Mwenda ni Naibu Mkuu wa upelelezi mkoa wa Njombe

 
 


Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia  Matrida Chaula na Dominicus  Luoga Kwa Mahojiano  Kuhusika na Matukio Mawili Tofauti ya Mauwaji Kati ya Matuko Manne Vifo Yalitokea Mkoani Njombe.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi Iliyotolewa Kwa Vyombo Vya Habari Inasema Kuwa Mtuhumiwa Matrida Chaula Mkazi wa Kijiji cha Mago Wilayani Makete anashikiliwa  na Jeshi Hilo kwa  mahojiano Kufuatia Kifo cha Frank Tisimia Sanga Aliyekutwa Amefariki Chumbani Kwa Mtuhumiwa Baada ya Kuchomwa na Kitu Kinachodhaniwa Kuwa  ni Kisu Sehemu za Kifuani na Yohana Sanga, Ambae Alitoroka Baada ya Kufanya Tukio Hilo.

Taarifa Hiyo  ya Jeshi la Polisi Pia imesema kuwa jeshi hilo Linamshikilia Dominicus  Luoga  Mkazi wa kijiji cha Ibumi Wilayani Ludewa Kwa Mahojiano Juu ya Mauwaji ya Jane Luoga Aliyeuwawa  Baada ya Kuchomwa na Kitu Kinachodhaniwa Kuwa   ni Kisu Sehemu za Shingoni.

Wakati Huo Huo Taarifa Hiyo Imeeleza Kuwa Watu Wanne Wamefariki Kutokana na Ajali za Barabara Ikiwemo Ile Iliyotokea Barabara ya Makambao Iringa  Ambapo Gari Ambalo Halikufahamika Namba za Usajili Liliwagonga Wapanda Baiskeli Gerald Kiwale na Joseph Ng'ande Wote Wakiwa Wakazi wa Idofi na Kusababisha Vifo Vya Watu Hao

Katika Ajali Nyingine Ilitokea Wilayani Ludewa na Kusababisha Vifo Vya Watu Wawili Akiwemo Matokeo Luoga Aliyefariki Akiwa Anapatiwa Matibabu Katika Hospitali ya Lugalawa na Jafari Luoga Aliyefariki Papo Hapo Baada ya Kugongana na Pikipiki Walizokuwa Wakiendesha.

Kwa Mujibu wa Taaarifa Hiyo iliyosainiwa na   kaimu afisa wa upelelezi mkoa wa Njombe Frolence  Mwenda imeeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Linaendelea na Uchunguzi Dhidi ya Matukio Hayo   Yaliyotokea Machi 17 Mwaka Huu.

Hata Hivyo Kaimu afisa upelelezi huyo Mwenda Ametoa Wito Kwa Madereva Kuendesha Vyombo Vyao Kwa Kufuata Sheria za Usalama Barabarani Ili Kupunguza Ajali Zisizo Za lazima Kwa Raia.

Hivi Karibuni Jeshi la Polisi Kwa Kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali  la APEC Lilitoa Mafunzo ya Usalama Barabarani Kwa Madereva wa Vyombo vya Moto Wilayani Njombe ,Mafunzo Yaliyotafsiriwa Kuleta Mafanikio Makubwa katika kupunguza Ajali za Barabarani  mkoani Njombe.

No comments:

Post a Comment