Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Titus Kamani Amezindua Kituo Chenye Tanki la
Kukusanya , Kupoza na Kuhifadhi Maziwa Lenye Thamani ya Shilingi Milioni 20 Katika Kijiji cha
Wangama Wilayani Njombe Kilichopo Chini ya Mtandao wa Vikundi Vya Wafugaji, Pamoja na
Kuwatembelea Wafugaji wa Ng'ombe Katika Kijiji cha Ibumila .
Akiongea Mara Baada ya Kuzindua Kituo Hicho Dkt. Kamani Amesema Kuwa Serikali Inatarajia
Kutoa Ng'ombe Elfu 40 wa Maziwa na Kuwagawa Katika Wilaya za Mkoa wa Njombe Likiwemo
Shamba la Kitulo Wilayani Makete Ikiwa ni Hatua ya Kuendelea Kuwaunga Mkono Wafugaji
Mkoani Hapa.
Waziri Huyo wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Amesema Serikali Imeanza Maandalizi ya
Kuanzisha Kituo Maalum Kwa Ukanda wa Nyanda za Juu Kitakacho Kuwa Sao Hill Ili Kupata
Mbegu Bora za Ng'ombe wa Maziwa , Huku Akiziagiza Halmashauri na Mamlaka za Mkoa Kusaidia
Kufuatilia Wawekezaji Binafsi Katika Uhamasishaji.
Keptain Mstaafu Aseri Msangi ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Changamoto
Kubwa Inayowakabili Wafugaji ni Ukosefu wa Mbegu Bora za Ng'ombe wa Maziwa na Kumuomba
Waziri Huyo Kuwasaidia Wafugaji Kupata Mbegu Hizo Bora za Ng'ombe wa Maziwa Huku
Akiwataka Wafugaji Kuwatunza Ng'ombe Wao Kwa Kuwapa Chakula cha Kutosha Ili Kupata
Maziwa Mengi.
Katika Risala Fupi Iliyosomwa Kwaniaba ya Wafugaji wa Kutoka Vijiji 11 Vya Wafugaji Wilayani
Njombe Imeeleza Kuwa Vijiji Vya Mtandao wa Wafugaji Vina Jumla ya Ng'ombe wa Maziwa Mia
669 na Kwamba Kati ya Hao Huzalisha Wastani wa Lita Elfu 2664 za Maziwa Kwa Siku.
Waziri Kamani Hapo jana Amehitimisha Ziara Yake ya Kikazi ya Siku Tatu Mkoani Njombe Kwa
Kutembelea na Kukagua Baadhi ya Miradi Mbalimbali Likiwemo Banda la Kufugia Nguruwe Katika
Halmashauri ya Mji wa Makambako Wilayani Njombe na Shamba la Mbuga ya Kitulo Wilayani
Makete.
No comments:
Post a Comment