KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CWT WILAYA YA NJOMBE BI SALAMA
LUPENZA AKITAFAKARI JAMBO WAKATI WA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO
ULIOFANYIKA LEO MJINI NJOMBE KATIKA UKUMBI WA CWT NJOMBE.
'"MWALIMU VIPI,TUTALIPWA KWELI MADAI YETU'"
BAADHI YA WALIMU WILAYANI NJOMBE WAKITAFAKARI JAMBO WAKATI WA MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CWT ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA CWT MJINI NJOMBE FEB 28 MWAKA 2014.
KATIBU WA CHAMA CHA WALIMU TANZANIA CWT WILAYA YA
NJOMBE BI SALAMA LUPENZA [ KULIA] AKISOMA TAARIFA YA KAZI ZA CHAMA HICHO
KATIKA KIPINDI CHA MWAKA 2010 HADI MWAKA 2013 LEO MJINI NJOMBE.
Chama Cha Walimu Tanzania CWT Wilayani Njombe Kimesema Kinaidai Serikali Zaidi ya Shilingi
Billioni Moja Kama Malimbikizo ya Malipo ya Mishahara,Likizo,Uhamisho na Stahiki Mbalimbali
Wanazostahili Kulipwa Walimu Hao Hadi Sasa.
Kutokana na Hali Hiyo Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilayani Njombe Kimeiomba Serikali
Kuwa Fikiria Na Kutekeleza Ahadi Zake Kwa Walimu Kwa Wakati ili Kuzima Migomo na Mivutano
ya Mara kwa Mara Inayojitokeza Kati ya Walimu na Serikali.
Aidha Chama Hicho Kimeiomba Serikali Kuendelea Kutatua Changamoto Zinazoikabili Sekta ya
Elimu Ikiwemo Uhaba wa Vyumba Vya Madarasa,Maabara Upungufu wa Walimu wa Masomo ya
Sayansi na Hisabati.
Akisom Taarifa ya Utekelezaji wa Kazi za Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Njombe
Kwa Kipindi Cha Juni 2010 Hadi June 2013 Katibu wa CWT Wilaya ya Njombe Bi Salama Lupenza
Amesema Pamoja na Mambo Mengine Suala La Motisha Kwa Walimu Wanaofanya Kazi Katika
Mazingira Magumu Pamoja na Kutatua Kero za Walimu Hasa Katika Ngazi ya Wilaya na Mkoa
Nalo Linapaswa Kuangaliwa na Serikali Kwa Umakini.
Amesema Mwezi Novemba Mwaka 201o CWT na Serikali Walifanya Uhakiki na Kupatikana Jumla
ya Shilingi Bilioni 53 Ambapo Kati ya Fedha Hizo Shilingi Bilioni 19 Zilikuwa za Walimu Waliopo
Chini ya TAMISEM.
Ameongeze Kuwa Madai Mengine ya Walimu ni Pamoja na Bilioni Tatu za Walimu Waliopo Chini
ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Pamoja na Shilingi Billioni 22
Zinazohusiana na Mishahara
Amefafanua Kwenye Taarifa Hiyo Kuwa Licha ya Serikali Kuendelea Kulipa Madai Hayo Bado
Imeshindwa Kulipa Madai ya Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu na Wakaguzi Kama Ilivyotarajiwa
Akizungumzia Changamoto Zinazokikabiri Chama Hicho Bi Lupenza Amesema ni Pamoja na
Serikali Kulipa Madeni Kwa Idadi Ndogo Kila Mwezi.
Katika Hatua Nyingine Chama Hicho Kimewaagiza Walimu Kufuata Maadili ,Sheria ,Kanuni na
Taratibu Zote za Kazi ya Ualimu Ili Kupunguza Kasi Kubwa ya Walimu Kufuzwa Kazi na Pengine
Hata Utumishi.
Akifungua Mkutano Huo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amesema Serikali Kwa
Kushirikiana na Walimu Katika Ngazi Tofauti Itaendelea Kutatua Changamoto na Kero Mbalimbal;i
Zinazowakabili Walimu Hapa Nchini.
Katika Hatua Nyingine Chama Hicho Kimemchagua Mwalimu Ambindwile Shaaban Kuwa
Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Njombe Wakati Bi Diana Nyemele Akichaguliwa Kuwa Mjumbe
Kitengo Cha Wanawake Ngazi ya Wilaya Pamoja na Mwalimu Agnes Kamba.
No comments:
Post a Comment