Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Monday, February 4, 2013

WANANCHI WA WILAYA ZA NJOMBE,MAKETE NA WANGING'OMBE KARIBU WATAMALIZIWA KILIO CHAO CHA KUKOSA MAHAKAMA KATIKA MAENEO YAO.





 Hii ni ofisi ya hakimu mkazi mkuu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe.
 
 Hakimu mkazi mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Njombe, makete na Wanging'ombe Augustini K. Rwanzile akiwa ofisini kwake.

Mahakama ya Hakimu Mkazi mwandamizi  Wilaya ya Njombe Inatarajia Kuzifanyia Ukarabati Mahakama za Vijiji Ikiwemo Mahakama ya Igominyi na Mdandu   Ikiwa ni Mpango Mkakati wa Kuboresha Huduma za Mahakama Kwa Wananchi wa Maeneo Hayo.

Aidha Mahakama Nyingine Zinazotarajiwa Kufanyiwa Ukarabati ni Pamoja na Mahakama ya Wilaya ya Wanging'ombe na Makete Ambazo Kwa Pamoja Wamekusudia Kuajiri Mahakimu Watakaofanya Kazi Katika Maeneo Hayo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Augustini Rwanzile Amesema Pamoja na Kuanzisha Mahakama Hizo Katika Maeneo Hayo Pia Wamekusudia Kuendelea Kutoa Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Uhalali na Haki ya Kutoa Ushahidi Pamoja na Muda Anaostahili Kutumikia Mahabusu Kwa Mtuhumiwa.


Kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania Yaliotarajiwa Kufanyika Feb 4 Mwaka Huu,Hakimu Rwanzile Amesema Maadhimisho Hayo Sasa Yatafanyika Feb 6 Mwaka Huu Huku Mgeni Rasmi Akitarajiwa Kuwa Mkuu wa mkoa wa Njombe.



Aidha Hakimu Rwanzile Anaweka Wazi Sababua za Kuahirishwa Kwa Maadhimisho Hayo Kutoka Tarehe 4 Hadi Kufanyika Tarehe 6 kwa kusema kuwa sherehe hizo huwa zinategemea na maelekezo toka kwa judge mkuu ambae huwaagiza mahakimu nchini kufanya sherehe hizo.

Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Njombe hususani wanaotokea vijijini wamesema kufuatia mikakati ya kufufua mahakama za mwanzo zilizoko maeneo mbalimbali ya vijiji endapo utekelezaji utakuwepo utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wa maeneo hayo ambao walitoka muda mrefu wakipata tabu ya kufuata huduma za kimahakama.

Pamoja na hayo wananchi hao wamekili kuwepo kwa baadhi ya watu kushindwa kufika kutolea ushahidi kutokana na uwezo mdogo wa kipato walionao  huku wakilalamikia kwamba wamekuwa wakitumia gharama kubwa za usafiri kwaajili ya kwenda kutoa ushahidi ambapo hali hiyo imefanya wengi wao kukataa kwenda kutoa ushahidi kutokana na kesi nyingi kuahirishwa kwa karibu siku zote.
Tatizo la mahakama na vituo vya polisi kukosekana kwa maeneo ya vijijini limeonekana kuwa ni miongoni mwa changamoto inayokabili maeneo hayo ambapo siku chache zilizopita wananchi wa kijiji cha Iwungiro wilayani Njombe walimuomba OCD wa jeshi la polisi Wilaya ya Njombe Lucy Mwakafwila alipobahatika kuwatembelea  kuwasogezea kituo cha polisi jirani nao kwa kusema huenda mauaji na uharifu mbalimbali ambao umekuwa ukijitokeza kijijini humo ukapungua.

No comments:

Post a Comment