Monday, February 4, 2013
WANANCHI NJOMBE WANUFAIKA NA SHIRIKA LA PADI KWA MIKOPO HUSUSANI WAZEE SHIRIKA HILO LA ENDELEA KUKOPESHA MIFUGO.
Wakuu wa idara,maafisa ustawi wa jamii,maendeleo na viongozi wa serikali za vijiji na kata wakiwemo madiwani.
Yohana Kalinga ni afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji wa Njombe akijibia kwanini wazee hawajapatiwa vitamburisho vya bima ya afya.
Mratibu wa shirika la PADI Wilaya ya Njombe Musa Mcharo akiwasilisha taarifa fupi ya shirika hilo.
Shirika Lisilo la Kiserikali la PADI Mkoani Nombe Limewaomba Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya ya Njombe Kuhakikisha Wanaharakisha Zoezi la Kuwapatia Vitambulisho Vya Matibabu Kwa Wazee Ili Kupata Fursa ya Kutibiwa Kwenye Vituo Vya Afya , Zahanati na Hospitali Kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii CHF.
Ombi Hilo Limekuja Kufuatia Malalamiko ya Baadhi ya Wazee Kutopatiwa Vitambulisho Hivyo Licha ya Kuwa Tayari Shirika Hilo Limetoa Fedha Katika Halmashauri za Mji na Wilaya ya Kwa Ajili ya Matibabu ya Wazee Hao Toka Mwaka 2011.
Aidha Mratibu wa PADI Taifa Bwana Isaka Msigwa Amemuomba Katibu Tawala wa Mkao wa Njombe Kuwaagiza Wakurugenzi wa Wilaya za Mkoa Huu Kuwaagiza Viongozi wa Kata na Vijiji Kuwashirikisha Wazee Kwenye Vikao Vya Maamuzi ya Serikali, Ambapo Kwasasa Shirika Hilo Liko Kwenye Mchakato wa Kuunda Mabaraza ya Wazee.
Bi. Yohana Kalinga ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Ambaye Amekiri Halmashauri Hiyo Kupokea Fedha Hizo na Kuwepo Uchelewashwaji wa Vitambulisho Vya Matibabu Vya Wazee Hao , na Kueleza Kuwa Wakati Wowote Kuanzia Sasa Watapatiwa Vitambulisho Hivyo.
Aidha bi Kalinga amesikitika kuona muavuli wa shirika la NJODINGO kwa kutofika katika semina hiyo licha ya kupewa taarifa na kuyataka mashirika mengine yasiyo yakiserikali kuiga mfano wa shirika la PADI katika jitihada mbalimbali za kuhakikisha yanafanikisha shughuli zao wanazofanya.
Amesema mkoa wa Njombe una mshirika mengi yasiyo yakiserikali lakini bado hayajaonesha kikamilifu ushiriki wake kwa jamii ambapo ameyataka mashirika hayo kushirikiana ili kuhakikisha yanafanikisha mahitaji ya wananchi husika kama linavyofanya shirika la PADI.
Nao Wazee Waliohudhuria Kikao Hicho Kutoka Halmashauri za Mji na Wilaya yaNjombe Wamelishukuru Shirika Hilo KwaKuwasaidia Kutetea Haki za Wazee na Misaada Kwa Ajili ya Kujiendeleza Kimaisha.
Awali akisoma taarifa ya shirika la PADI Mratibu wa shirika hilo Wilaya ya Njombe bwana Musa Mcharo amesema shughuli mbazo shirika hilo limekwisha kufanya tangu mwaka 2011 hadi mwaka 2012 kuwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 na uundaji wa mabaraza ya wazee katika ngazi ya kata na vijiji.
Pia amesema shirika hilo limefanya kazi ya kuelimisha vikundi 30 vya wakusanya takwimu na taarifa za wazee ambavyo vipo ndani ya kata ya Yakobi,Ramadhani,Makoga,uwemba,Mtwango na Mjimwema, huku wazee 80 wakipewa mikopo yenye mashariti nafuu ya 5% yenye thamani ya shilingi 5,200,000 kwa kata ya Yakobi na Makoga ambapo kila mzee alipata shilingi elfu sitini na tano.
Pamoja na hayo Mcharo amesema shirika hilo limetoa mikopo ya kuku na Mbuzi kwa wazee 114 wa kata ya Mtwango na Yakobi katika vijiji vya Lunguya na Itunduma kata Mtwango,na vijiji ya Yakobi na Nundu ambapo jumla ya mbuzi 193 na kuku 206 walikabidhiwa wazee hao.
Tayari Shirika Hilo Limetoa Misaada Mbalimbali Kwa Wazee wa Halmashauri za Wilaya na Mji wa Njombe Ikiwemo Misaada ya Fedha , Mifungo Pamoja na Kuwalipia Huduma za Matibabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment