Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, February 28, 2013

POLISI MAKETE WAUA MTEJA WA BENKI KWA RISASI , MUUWAJI AKAMATWa.


Askari  wa  FFU mkoani Iringa  wakimwadhibu kwa  kipigo aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten mkoa  wa Iringa marehemu Daudi Mwangosi (wa  pili kushoto) kabla ya  kuuwawa kwa bomu septemba 2 mwaka 2012 katika  kijiji  cha Nyololo Mufindi.(picha na maktaba ya mtandao huu)  
.....................................................................................................................................................................
WAKATI  mtuhumiwa  wa  mauwaji ya aliyekuwa mwandishi  wa kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa  Daudi Mwangosi askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani  leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari  wilaya ya Makete  mkoa wa Njombe  wadaiwa  kufanya mauwaji ya  kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi .
Huku  askari  askari  mmoja nayetuhumiwa kufanya  unyama  huo aliyetambulika kwa  jina moja la Jose akishikiliwa na  jeshi  la  polisi kufuatia mauwaji hayo ya  kinyama.
Tukio  hilo  limekuja  huku  bado watanzania   hasa  wakazi  wa  mikoa  ya Iringa  na Njombe  wakiwa bado hawajasahau  mauwaji ya  kinyama  yaliyomkuta  mwanahabari Daudi Mwangosi  ambapo kesi hiyo  bado ikiendelea kutajwa na  wanahabari waliokuwepo eneo la tukio  siku ya mauwaji  wakisubiri  kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi  wa kesi hiyo pindi  itakapoanzwa kusikilizwa.
Mwandishi  wa mtandao huu   kutoka  Makete  Njombe anaeleza  kuwa   tukio  hilo  wamedai kuwa  mauwaji hayo ya  kinyama  yametokea jana  jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja  huyo aliyekuwa na  usafiri  wa  boda  boda  kufika  eneo hilo la  benki kwa lengo la  kuchukua  fedha  .
Imedaiwa  kuwa  aliyepigwa  risasi anatambuliwa  kwa  jina la Casto  Kawambwa  mkazi  Mbalizi  mkoani Mbeya  na kuwa  baada ya  kupigwa  risasi alikimbizwa  katika  Hospitali ya  wilaya ya Makete  ambako inadaiwa kabla ya  kupatiwa matibabu amefariki  dunia  .
Kutokana na tukio hilo  jeshi la  polisi  liliwazuia  wanahabari  kutimiza  wajibu  wao kwa  kupiga  picha  wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake  kuweka  ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili  kuzuia  wanahabari  kusogea  eneo hilo .
 Hata  hivyo  mmoja kati ya  askari ambae   jina lake halikufahamika mara  moja alisikika  akidai kuwa  chanzo cha mteja  huyo wa benki  kupigwa  risasi  alikuwa akihisiwa  kuwa ni jambazi na  hivyo  baada ya  kufika  eneo hilo  kwa usafiri  wake wa  piki  piki (boda boda )  walihisi kuwa amefika  kwa ajili ya  kufanya  vitendo vya uporaji katika  benki  hiyo na hivyo  askari katika hali ya  kujihamia aliamua  kumpiga  risasi .
Jitihada za  kumtafuta  kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Njombe  ili  kuzungumzia  undani  wa  tukio  hilo  linafanyika na mtandao huu .

No comments:

Post a Comment