Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Wednesday, February 27, 2013

BUNGE LA TANZANIA KUSHIRIKIANA KWA KARIBU NA BUNGE LA NAMIBIA.


aSpika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (kushot)  akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Namibia nchini Tanzania Balozi Japhet Issack alipomtembelea ofisini kwake leo.Pamoja na mambo mengine Balozi huyo amemuomba Spika Makinda kuimarisha uhusiano  na Bunge la Namibia kwani kuna mambo mengi Bunge hilo linaweza kujifunza kutoka Tanzania.
b Spika Makinda akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Balozi wa Namibia nchini Tanzania ambapo amemhakikishia Balozi huyo kuwa Bunge la Tanzania lipo tayari kushirikiana na Bunge la Namibia na kuona ni maeneo yapi ambayo yatawafaidisha wananchi wa  nchi mbili hizi. Aliainisha maeneo ya mafunzo na kujenga uwezo kuwa ya kipaumbele.
Na Prosper Minja-Bunge.

No comments:

Post a Comment