Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Saturday, February 23, 2013

BAADHI YA NYUMBA ZA MTAA WA KIHESA ZILIZOJENGWA KANDO YA MTO ZIPO MBIONI KUKUMBWA NA MAFURIKO YA MAJI,WAMILIKI WA NYUMBA MBILI WAAMBIWA WAHAME TOKANA NA KUWA KATIKA MAENEO HATARISHI KATIKA MTAA WA MPECHI NA JOSHONI.





Daraja hili limekreki mpaka aliko simama kijana aliyeshika mfuko mkononi.



Daraja la mtaa wa Kihesa mjini Njombe eneo la kwa Makinda lipo  mbioni kukumbwa na maji kutokana na maji na hawa ni wananchi wa mtaa wa Kihesa wanashangaa  baada ya mvua kubwa kunyesha.









Hiz ni nyumba za mtaa wa Kihesa zipo mtoni kabisa na viwanja hivi vilipimwa na maeneo mengine yanakataliwa lakini wananchi wenyewe wanaamua kujenga pasipo kuangalia maisha ya mbele.


Hizi ni nyumba zipo kando ya mto je zitapona na mafuriko  hali hii imetokea siku chache silizopita lakini imedaiwa viwanja hivi  vimepimwa.



Ilikuwa kazi kweli kweli wakazi wa nyumba hizo wakati mvua ikinyesha amani ilitoweka jinsi maji yalivyokuwa yakitililika kwa wingi.



Wananchi wa mtaa wa Kihesa  waitaka serikali ya halmashauri ya mji wa Njombe kuwajengea madaraja katika mtaa huo ili wanafunzi na magari yaweze kuvuka pasipo  mashaka yoyote .

Wakizungumza na matukio wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba serikali yao iwaboreshee miundombinu ya madaraja lakini bado hadi sasa.

Ombi hilo limefruatia kuharibika kwa miundombinu ya madaraja na barabara ambapo pamoja na hayo wamesema katika daraja la kihesa eneo la kwa makinda nguzo zake zimeoza muda wowote zinaweza kuvunjika endapo magari makubwa yataendelea kupita.

Muhandis wa halmashauri ya mji wa Njombe bwana Kaogoamesema halmashauri ipo kujipanga kwenda kutatua tatizo hilo la ujenzi wa daraja la kwa Makinda huku akisema halmashauri inatarajia kujenga madaraja mbalimbali yanayozunguka ikiwemo la Mabatini.

Aidha bwana Kaogo amewataka wananchi kuwa wavumilivu na kusema wahakikishe magari yenye zaidi ya tani kumi yasipite katika daraja hilo kama  serikali inavyozuia magari makubwa kupita barabara zenye kiwango cha kokoto kutokana na kuharibika mapema.

No comments:

Post a Comment