Friday, January 18, 2013
MAONI YAENDELEA KUTOLEA NA BAADHI YA WADAU JUU YA SENZA NA GESI MTWARA
Mwenyekiti wa chama cha TLP Wilaya ya Njombe Lukule Mponji akiwa ofisini kwake.
Wakati Matokeo Zaidi ya Sensa ya Watu na Makazi Yakitarajiwa Kutolewa Baadae Mwaka Huu,Chama Cha TLP Wilayani Njombe Kimekuwa na Maoni Tofauti Kuhusu Matokeo ya Awali Yaliotangazwa na Rais Jakaya Kikwete Dec 31 Mwaka Jana.
Aidha Chama Hicho Kimetaka Kuwepo Kwa Serikali Tatu Ikiwemo Serikali ya Tanganyika,Zanzibar na Ile ya Muungano Kwa Kuwa Zanzibar Imeendelea Kutambulika Kama Taifa Likiwa na Rais Wake Licha ya Kujiunga na Tanganyika na Kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Akizungumza na Uplands Fm,Mwenyekiti wa Chama Cha TLP Wilaya ya Njombe Bw Lukule Mponji Amesema Kitendo Cha Kuendelea Kuwa na Uwakilishi Sawa na Vyombo Mbalimbali Zikiwemo Kamati za Kitaifa Bila Kujali Idadi ya Watu Waliopo Baina ya Pande Hizo ni Sawa na Watanganyika Kuendelea Kujisaliti
Kuhusu Uteuzi wa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Ambayo Kwa Mujibu wa Matokeo Hayo Haukupaswa Kuwa Wenye Uwiano Sawa Kati ya Tanzania Bara na Zanzibar Jambo Ambalo Linaweza Kuwa na Athari Kubwa Endapo Mabadiliko Hayo ya Katiba Yatahitaji Kuridhiwa na Pande Zote.
Kwa Sasa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Imekuwa Ikipokea Maoni ya Makundi Maalum Vikiwemo Vyama Vya Siasa Ambavyo Vimekuwa na Maoni Tofauti Ikiwemo Vile Vinavyotaka Kupunguzwa Kwa Madaraka ya Rais na Uwepo wa Serikali Tatu
Dec 31 Mwaka Jana Rais Kikwete Alitangaza Matokeo ya Awali ya Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Iliofanyika Mwezi Agost Hadi Sept Mwaka Jana Ambapo Idadi ya Watanzania Ilitajwa Kufikia Millioni 44.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment