Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Friday, January 18, 2013

MTUHUMIWA MMOJA WILAYANI MAKETE AJINYONGA NA KAMBA YA KAPUTULA ALIYOKUWA AMEIVAA NDANI YA CHUMBA CHA MAHABUSU.

 RPC Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani akiwa ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari.

Mkazi Mmoja wa Kijiji cha Isapulano Wilayani Makete Mkoani Njombe Chuki Zawadi Semwa Amekutwa Amejinyonga Kwa Kutumia Kamba ya Kamptula Aliyokuwa Ameavaa Akiwa Mahabusu  Katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Makete Jana Asubuhi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo na Kueleza Kuwa Marehemu Alifikishwa Katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Makete Jana Majira ya Saa 1:30 Usiku Akituhumiwa Kuvunja Nyumba Mbili Tofauti na Kuiba Vitu.

Amesema Mwili wa Marehemu Tayari Umezikwa Mara Baada ya Kufanyiwa Uchunguzi wa Kitabibu.



Wakati Huo huo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limesema Kuwa Usalama Katika Vyombo Vya Usafiri Mkoani Hapa Utategemea Zaidi Ushirikiano Kati ya Wananchi na Madereva wa Vyombo Hivyo Kwa Kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani Pamoja na Wananchi Wenyewe.

Aidha Jeshi Hilo Limewataka Wananchi Kufahamu Kuwa Usalama Wao Kwenye Vyombo Hivyo Uko Chini ya Uamuzi Wao Kwa Kukataa Kutumia Magari Yanayoonekana Kujaa Abiria Wengi Kwa Wakati Mmoja Kwa Kuwa Jambo Hilo Pia Huweza Kusababisha Ajali na Kusababisha Madhara Kwa Wananchi.

Akizungumza na Uplands Fm,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Fulgency Ngonyani Amesema Kutokana na Kukua Kwa Sekta ya Usafirishaji Mjini Njombe ni Vema Wahusika Wakatambua Haki ya Ulinzi na Usalama Kwa Kila Mtumiaji wa Chombo Kinachotoa Huduma ya Usafiri.

Ameongeza Kuwa Jeshi la Polisi Bado Linaendelea Kutoa Elimu Kwa Wananchi Juu ya Namna ya Kutoa Taarifa Zinazohusu Ukiukwaji wa Sheria za Usalama Barabarani Unaoendelea Kufanywa na Baadhi ya Madereva

No comments:

Post a Comment