Pages

CONTACT

0757092504/0678321772

Thursday, January 17, 2013

THE MIC KING: SADAM OUT, WATATU DANGER ZONE!

Photo: THE MIC KING: SADAM OUT, WATATU DANGER ZONE!
MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid  ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone).
Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao.
Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam (pichani)kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone.
Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati  wakijinadi runingani.

MSHIRIKI wa Shindano la The Mic King lililoendelea kutimua vumbi kila Jumapili katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala Zakhem jijini Dar, Sadam Rashid  ‘KM 18’ ameliaga shindano hilo huku washiriki wengine watatu wakiingia kwenye eneo la hatari (danger zone). 
 
Awali, wasanii wawiliwawili kutoka katika makundi ya Risasi, Championi, Uwazi na Ijumaa waliwasilisha jukwaani kazi walizokuwa wamepewa huku majaji wa shindano hilo, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, Ally Baucha na John Dilinga ‘DJ JD’ wakitoa komenti zao. 
 
Mwishoni, MC wa shindano hilo alimtangaza Sadam kuwa ametolewa kutokana na kupata kura chache kutoka kwa watazamaji huku Hamza ‘KM 11’, Paizo ‘KM 17’ na Salum ‘KM 20’ wakitangazwa kuingia kwenye danger zone. 
 
 Shindano huoneshwa kila Jumanne saa nne usiku katika Runinga ya DTV na marudio ni Alhamisi saa 10 jioni na Jumamosi kuanzia saa 8 mchana ambapo mashabiki hupata fursa ya kuwapigia kura washiriki wakati  wakijinadi runingani.Imeandaliwa na mdau wa matukio toka Iringa Francis Godwin.

No comments:

Post a Comment