Monday, January 21, 2013
MCHUNGAJI TWEVE WA KANISA LA TANZANIA ASSEMBLES OF GOD AWATAKA WACHUNGAJI KUTOA ELIMU YA UJASILIAMALI KWA WAUMINI ILI KUJIKWAMUA NA HALI YA UMASIKINI NA KUMTUMIKIA MUNGU KWA MOYO WOTE.
Hili ni kanisa la Tanzania Assebles Of God linapatikana Melinze mjini Njombe hapa waumini wapo kanisani wanapokea neno la Uzima.
Mchungaji Cefania Tweve akitoa huduma ya maombezi kwa baadhi ya waumini waliookoka na wanaookoka.
Waumini wa kanisa la TAG Melinze wakishuhudia miujiza na maombi makubwa yanayofanywa na mchungaji na watumishi wengine wa Mungu.
Hapa waumini wanatoka kanisani kuelekea nyumbani kwao baada ya kushibishwa na neno la Enjili kanisani humo.
Viongozi wa Dini Mkoani Njombe Wametakiwa Kutoa Elimu ya Uchumi na Namna ya Kujiongezea Kipato Miongoni Mwa Waumini Wao Badala ya Kuendelea Kujihusisha na Mambo ya Kuwadanganya Waumini na Kujihusisha na Imani Potofu.
Akizungumza kwenye ibada ya jumapili ya jana Mchungaji wa Kanisa la TAG Njombe Mchungaji Zephania Tweve Amesema Miongoni Mwa Shughuli za Kiuchumi Zinazoweza Kuhamasishwa na Viongozi Hao ni Pamoja na Kilimo na Biashara Mbalimbali Kuliko Kuendelea Kuamini Katika Maendeleo ya Uchumi Kwa Kutegemea Nguvu za giza.
Amesema ili waumini wanufaika na uchumi uliopo na kuweza kumtumikia Mungu ni vema waumini wakatambua umuhimu wa kujishughulisha katika kazi kwa kuwa na miradi mbalimbali ya kimaendeleo itakayo wasaidia kujikwamua na hali ngumu ya umasikini katika eneo husika anapoishi.
Mchungaji Tweve amesema kwa kufanya hivyo itasaidia waumini kuhubiri neno la Mungu kwa nguvu zote na kuivuta jamii nyingine ambayo bado haijatambua nini maana ya kulihubiri neno la Mungu na namna ya kuepukana na matendo ovu ambayo yamendelea kukithili hapa duniani.
Pamoja na hayo Mchungaji huyo ametoa wito kwa waumini kushirikiana na serikali katika kupambana na matendo mabaya ya ujambazi,uzinzi,ulevi na namna yakuwarekebisha watoto na vijana ambao wameingia katika ulimwengu wa utandawazi.
Kwa upande wake mkuu wa Idara na maandiko katika kanisa la TAG Melinze Samwel Mlowe Amekemea Tabia ya Baadhi ya Waumini Kujihusha na Masuala ya Siasa na Kusema Kuwa Waumini Wanapaswa Kuwa Makini Kwa Kutochanganya Mambo ya Siasa na Dini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment