HUYU ni mkurugenzi mtendaji wa kituo cha maendeleo ya kilimo na ufugaji Lupembe mchungaji Charles Mwantepele.
Wakati serikali ikirejesha mfumo wa elimu ya kujitegemea mashuleni kituo cha maendeleo ya kilimo na ufugaji kilichopo Lupembe wilayani Njombe kimeanza kutoa elimu ya ujasiliamali Kwa wanafunzi wenye umri wa kuanzia miaka 6 hadi 25 kupitia mradi wa 4H.
Akizungumza na kituo hiki mkurugenzi mtendaji wa kituo cha maendeleo ya kilimo na ufugaji Lupembe mchungaji Charles Mwantepele amesema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia wanafunzi wa shule za sekondari na Msingi katika kuboresha na kuinua kiwango cha elimu kupitia elimu ya kujitegemea.
Mchungaji Mwantepele amesema kuwa mradi huo pia umelenga kupunguza wimbi la vijana kukimbilia mijini mara baada ya kufeli mitihani yao badala yake wajishughulishe na ujasiliamali mbalimbali katika maeneo yao ili kujikwamua na suala la kiuchumi.
Amesema kuwa Mradi wa [4h]yaani Head,heart,Hands and Health ni mradi unaolenga kuwafundisha vijana kutumia viungo vya mwili kama Kichwa,Moyo,Mikono pamoja na afya katika kufanya kazi za kibunifu ili kuwasaidia katika maisha yao ya baadaye.
Amesema tayari zaidi ya shule kumi za msingi na Sekondari zimesha fikiwa kupitia elimu ya mradi huo katika mmajimbo yote ya Wilaya ya Njombe na wilaya jirani za mkoa wa Iringa na Mbeya ambao matarajio ni kuinua kipato kupitia ubunifu na ujasiliamali tangu wakiwa wadogo.
Hata hivyo amezitaja shule hizo kuwa ni zile za Sekondari na msingi zikiwemo za wilaya ya Mufindi huko mafinga na Wilaya ya Mbalali mkoani Mbeya.
Miongoni mwa elimu ya Ujasiliamali inayotolewa kwa wanafunzi hao ni pamoja na ufugaji wa kuku.Simbilisi,kupanda miti ya matunda,kutunza bustani Ndogondogo kuwafundisha taalamu hya kuzungumza mbele za watu ili kuja kuwafundisha wenzao.
No comments:
Post a Comment