Wajumbe wa baraza la madiwani kwa awamu ya kwanza kwa kuanza na mfumo mpya wa madiwani kuwasilisha taarifa za kata.
Madiwani wakipitia taarifa za kata kabla ya kuwasilisha kwenye baraza hilo leo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe bwana Paulo MALALA ambaye alikuwa katibu wa kikao cha madiwani leo akiongoza kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao cha baraza kwa kuanza na uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya kata zao.
Madiwani wakitoka majira ya saa Moja kasoro jioni ya leo mara baada ya kikao hicho kuahirishwa na kuendelea mapema kesho kabla ya baraza la kawaida kuanza.
Kwa
mara ya kwanza madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe na
Wanging'ombe wameanza kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika kata zao
Katika uwasilishwaji wa taarifa
hizo kata ya Mtwango imekuwa ya kwanza kuwasilisha taarifa yake
ikiwasilishwa na afisa mtendaji wa kata hiyo bwana Jimson Mwanza kwa
niaba ya Diwani ambaye ni mwenyekiti wa halmashauri bwana Valence
Kabelege ambapo naye alishindwa kufika katika kikao hicho kwa sababu
zisizozuilika.
Aidha taarifa ya kata hiyo imeiomba halmashauri
kutoa elimu ya utawala bora kwa viongozi waliochaguliwa hivi karibuni
kutokana na vongozi wengi kudaiwa kutokuwa na elimu hiyo.
Kata ya
kipengele imeonekana kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya kesi
za baraza la ushauri kuliko kata nyingine zote zilizowasilisha taarifa
zao kwa siku ya jana huku Diwani wa kata ya Kipengele Bwana Lukemelo
Mgaya amesema jumla ya kesi 31 zimeshughulikiwa
kwa kupata mapato ya zaidi ya shilingi milioni moja huku kata nyingine
zikionekana kuwa chini kimapato katika suala la mashauri
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Igongolo bwana Ayoub Mkane amesema kuwa
zaidi ya shilingi milioni nane zilipatikana katika makusanyo ya kipindi
cha miezi mitatu huku Fedha hizo zikiwa zimekusanywa kutoka kwenye
vyanzo mbalimbali ikiwemo biashara ya pombe za
kienyeji,Mbao,mazao,vioski,ukaguzi wa nyama huku baraza likiwa na jumla
ya kesi tano tu kwa kipindi hicho.
No comments:
Post a Comment