Wanafunzi wa shule ya sekondari Njombe wakiekiti sauti za viongozi wao wa shule siku ya mahafali ya kidato cha sita.
Hapa ni shangwe na nderemo vijana wa Njombe sekondari wakitumbuiza kwa sarakasi na michezo mbalimbali.
Anaitwa Mgala Maurid maarufu kama Barlkiss king Jay na wimbo wake wa rap wa weekend akiburudisha umati wa watu waliohudhuria mahafari hiyo Njombe sekondari.
Na huu nao ni mtindo wa burudani za vijana wanacheza kwa stepu bila kumkanyaga mwenzie.
Mkuu wa shule ya sekondari Njombe {NJOSS } Benard William Akisoma taarifa fupi ya shule.
Mgeni rasmi afisa elimu mkoa wa Njombe Said Kinyaga Nyasiro akitoa hotuba kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Njombe Mgen Baruani.
Robin Mwakalinga akiwa ni mzazi alizungumza kwa niaba ya wazazi wote waliohudhuria mahafari hayo.
Maria Mloge ni mwenyekiti wa shule ya sekondari Njombe NJOSS akitoa nasaha kwa waagwa na waaga pamoja na wazazi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Mgeni Baruani Amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Shule ya Sekondari Njombe NJOSS Inapata Hati Miliki ya Ardhi na Kumaliza Mzozo Uliopo Kwa Sasa Kati ya Uongozi wa Shule Hiyo na Wananchi
Agizo Hilo Linafuatia Taarifa ya Maendeleo ya Shule Iliosomwa na Mkuu wa Shule Hiyo Ambayo Pamoja na Changamoto Nyingine Zinazoikabili Shule Pia Ilielezea Namna Shule Hiyo Inavyokwama Katika Mipango Yake ya Kimaeneleo Kutokana na Kukosa Hati Miliki.
Akizungumza Kwa Niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe Wakati wa Mahafali ya Kumi na Moja ya Kidato Cha Sita Shuleni Hapo Afisa Elimu Mkoa wa Njombe Kwa Shule za Sekondari Bw Said Nyasiro , Amesema Pamoja na Agizo Hilo Pia Ofisi Yake Itatoa Kiupambele Kwa Shule Hiyo Wakati wa Ugawaji wa Walimu Wapya Wanaoatarajiwa Kujiriwa Mwezi Ujao.
Awali Akizungumza Kwenye Mahafali Hayo Mkuu wa Shule ya Sekondari Njombe Bwana Benard William Ameipongeza Serikali Kwa Jitihada Zake za Kuendelea Kutatua Baadhi ya Changamoto Zinazoikabili Shule Hiyo Ikiwemo Ukarabati wa Samani na Vifaa Vingine.
Aidha mkuu huyo wa shule bwana William amesema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1953 ikiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne na mwaka 2001 ilianzisha madarasa ya kidato cha tano na cha sita na kusema kuwa idadi ya wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi imeongezeka hivyo ameomba serikali kuwasaidia kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo ya walimu,nyumba za walimu,usafiri , ukarabati wa mabweni na kupatiwa tanakrishi ili kuendana na mfumo wa sayansi na technolojia.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi waliohudhuria katika mahafari hayo jana january 23 Robin Mwakalinga amepongeza kwa jitihada zinazofanywa na walimu waa shule hiyo na kusema kuwa wazazi wanajukumu la kuonesha ushirikiano katika kuwalea watoto wakiwa shuleni na nyumbani ili wanafunzi hao wapate urahisi wa kupata ajira mara baada ya kumaliza elimu ya sekondari na chuooni.
Akisoma risala fupi kwaniaba ya wanafunzi wote wa kidato cha sita Gwakisa Mwanja amesema walianza kidato cha tano wakiwa na jumla ya wanafunzi mia tano na nane na sasa wanahitimu wakiwa mia tano na nne kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuhama,kupata matatizo ya kiafya na utoro.
Amesema shule hiyo imefanikiwa kuboresha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu,riadha,kikapu pamoja na kuboresha nidhamu shuleni kutokana na kuwepo kwa walimu wanaofuatilia nidhamu nzuri hali iliyofanya utovu wa nidhamu kupungua shuleni hapo.
Aidha Gwakisa amesema shule hiyo imefanikiwa kutunza mazingira kwa kupanda maua na miti pamoja na kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka shule hiyo mara kwa mara huku wakitaja kuwa shule hiyo inajishughulisha na upandaji wa miti ya matunda na mbao ambapo mwaka 2011 walifanikiwa kupanda miti elfu kumi ya mbao na mwaka huu 2013 wanatarajia kupanda miti elfu tano ya mbao ili kukuza uchumi wa shule hiyo.
Jumla ya Wanafunzi Mia Tano na Nne Wanatarajiwa Kuhitimu Kidato Cha Sita Mwaka Huu Katika Shule ya Secondary Njombe ambapo Kauli mbiu ya shule ya sekondari Njombe inasema Elimu ni Ukombozi.
No comments:
Post a Comment