Capt.Mstaafu Asseri Msangi,akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Sarah Dumba mwishoni kulia ni mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi wakiwa kwenye kikao cha Utekelezaji wa Ilani mkoa wa Njombe.
TAARIFA YA MAFANIKIO
YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM KUANZIA
MWAKA 2005 – 2012 ILIYOSOMWA NA MKUU WA MKOA MHESHIMIWA KAPT. (MSTF) ASERI
MSANGI
TAREHE 7 JANUARI 2013
Ndugu
Wananchi;
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kutufikisha kuuona Mwaka Mpya wa 2013 tukiwa wazima na Afya njema.
Pili napenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zangu
za dhati kwa wananchi wa Mkoa wa Njombe pamoja na Wadau wa Maendeleo kwa
kushiriki kwao kwa namna mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za Maendeleo
na Utoaji wa huduma Mkoani kwetu. Hotuba
yangu leo inahusu Mafanikio ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa
kipindi cha 2005 – 2012.
Ndugu Wananchi;
Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005 na
2010, Wananchi wa Mkoa wa Njombe wamefanya shughuli mbalimbali za Kiuchumi na
Kijamii. Aidha, shughuli kuu ni pamoja
na Kilimo, Ufugaji, Upasuaji wa Mbao, Uvuvi, Biashara, Ajira za Maofisini na
Viwandani. Sambamba na shughuli hizi, usimamizi na ufuatiliaji katika Mamlaka
za Serikali za Mitaa umeimarishwa ili kuhakikisha kuwa huduma kwa wananchi
zinaboreshwa. Mafanikio yaliyopatikana
katika sekta mbalimbali ni kama ifuatavyo:-
1.0 UTAWALA BORA
Ndugu Wananchi;
(i) Maeneo Mapya ya Utawala
Mnamo tarehe
1 Machi 2012 Serikali
ilitangaza rasmi kuanzishwa kwa Mkoa wa Njombe ukitokea Mkoa wa Iringa na kutangaza katika Gazeti la Serikali Toleo Namba
9 la mwaka 2012. Sanjari na
kuundwa Mkoa, Serikali ilitangaza kuanzishwa
kwa Wilaya ya Wanging’ombe ikitokea
katika Wilaya ya
Njombe. Aidha, Serikali ilianzisha Halmashauri ya
Mji wa Njombe katika mwaka 2007
na mwezi Julai 2012 Halmashauri
ya Mji wa Makambako ilianzishwa.
Imeandaliwa na mdau wa matukio Gabrie Kilamlya.
No comments:
Post a Comment