Thursday, April 13, 2017
UWANJA WA SABASABA KUKARABATIWA NJOMBE
NJOMBE-MICHEZO
Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Njombe Kimeunda Kamati Maalumu Ya Kusimamia Ukarabati Wa Uwanja Wa Mchezo Wa Mpira Wa Miguu Wa Sabasaba Itakayokuwa Chini Ya Viongozi Wa Chama Cha Mapinduzi Ili Kupata Uwanja Wa Michezo Unaokubalika Kwa Michezo.
Katibu Wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Njombe Sadakatt Kimati Amesema Kuwa Kamati Hiyo Itaanza Mara Moja Kuimarisha Uzio Wa Nje Wa Uwanja Wa Sabasaba Kwaajili Ya Kusaidia Kupata Mapato Kutokana Na Watazamaji Wa Michezo Ya Mpira Wa Miguu Itakayokuwa Inaendelea Katika Uwanja Huo.
Sadakatt Amesema Lengo La Kukarabati Uwanja Huo Ni Kuwezesha Shughuli Za Michezo Ya Mpira Wa Miguu Ya Kitaifa Kuendelea Njombe Mjini Njombe Ambapo Hadi Sasa Wamekwisha Jaza Mchanga Na Kupanda Nyasi Ambazo Tayari Zimekwisha Stawi Na Watajenga Uzio Wa Ndani Ya Uwanja Ili Kuzuia Watazamaji Wasiingie Ndani Wakati Mchezo Ukiendelea.
Kimatt Amesema Ujenzi Huo Unategemea Kuwepo Kwa Wahandisi Wa Ujenzi,Wafanyabiashara , Watu Wenye Taaluma Za Michezo Pamoja Na Maafisa Michezo Ambao Wapo Kwenye Kamati Hiyo Ili Kuanza Ukarabati Haraka Iwezekanavyo Kupata Uwanja Wa Michezo.
Bwana Kimatt Amesema Kufikia Mwezi Wa Saba Uwanja Wa Sabasaba Utakuwa Umekamilika Na Kuukabidhi Chama Cha Mpira TFF Kwaajili Ya Kutumiwa Na Timu Za Kitaifa Kwenye Ligi Kuu Zitakazo Kuwa Zinaendeshwa Nchini.
Amesema Kukarabatiwa Kwa Uwaja Huo Kutatoa Fursa Kwa Chama Hicho Kupata Mapato Kutokana Na Tozo Zitakazokuwa Zinachukuliwa Kwenye Uwanja Huo Kutoka Kwa Mashabiki Wa Mpira Wa Miguu Watakaokuwa Wanaingia Kwa Viwango Mbalimbali Vya Kiingilio .
Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Muda Wa Ukarabati Wa Uwanja Huo Frank Simon Msuya Amesema Chama Cha Mapinduzi Kama Mdau Wa Michezo Kimeamua Kuunda Kamati Ya Kusimamia Ukarabati Wa Uwanja Huo Ili Timu Ya Njombe Mji Ipate Fursa Ya Kuutumia Katika Mechi Mbalimbali Za Kitaifa.
Msuya Amesema Kuwa Uwanja Huo Umewekwa Kama Kitega Uchumi Kwa Chama Hicho Huku Wananchi Wa Njombe Njombe Nao Watanufaika Na Shughuli Mbalimbali Za Kibiashara Watakazo Kuwa Wanafanya Pindi Mechi Zinapochezwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment