Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga.
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.
Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.
Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.
“Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza
“Ili kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema
Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.
Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na wagonjwa wa Afya ya Akili.
“Niuombe uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika matumizi yake kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila ambapo kunahitajika msaada” alisema
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituo vinavyotoa huduma za Afya ya akili.
Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.
No comments:
Post a Comment