HILI NI ENEO ALA KITONGOJI CHA MALAMBA KIJIJI CHA USITA KATA YA ULEMBWE WILAYA YA WANGING'OMBE AMBALO MADINI YANAUNGUA AMBAYO YATAKUJA KUWA MAKAA YA MAWE BAADA YA MIAKA MILIONI MIA MBILI
WATALAAMU WA MADINI MKOA WA NJOMBE WAKITAFITI UMBALI ULIPO WA MOTO ULIOUNGUZA ENEO HILO MJIOLOJIA WA MADINI JOHN MAGANGA AKIWA NA WENZAKE.
WANANCHI WAKIFUKUA ILI KUPATA KINA AMBACHO MOTO UMEUNGUZA
WANGING'OMBE
Wananchi Wa Kijiji Cha Usita Kata Ya Ulembwe Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Wametakiwa Kuacha Shughuli Za Kijamii Katika Eneo La Madini Ambayo Baadaye Yanadaiwa Kuja Kuwa Makaa Ya Mawe Ili Kuepukana Na Madhara Yanayoweza Kujitokeza Ikiwemo Kutumbukia Kwenye Mashimo Yalioungua Na Moto.
Wakizungumza Na Kituo Hiki Baadhi Ya Wananchi Wa Kijiji Cha Usita Kitongoji Cha Malamba Wamesema Katazo Hilo Wamelipokea Na Kuahidi Kuacha Shughuli Za Kijamii Ambazo Walikuwa Wakizifanya Ikiwemo Uchomaji Mkaa Na Kuchungia Mifugo .
Wamesema Kutokana Na Watalaamu Wa Madini Mkoa Wa Njombe Kuwaomba Wananchi Kuacha Shughuli Za Uchomaji Mkaa Na Kuchungia Mifugo Katika Eneo Hilo Kwa Usalama Wao Sasa Watakuwa Walinzi Hata Kwa Watu Wengine Wasifanye Shughuli Eneo Hilo Hadi Litakapopatiwa Ufumbuzi Na Watalaamu Wa Madini.
Mwenyekiti Wa Serikali Ya Kijiji Cha Usita Abrahamu Mgaya Amesema Wakati Watalaamu Wa Madini Wakiendelea Na Uchunguzi Wa Kaboni Inayowaka Katika Eneo Hilo Ambayo Baadaye Itakuja Kuwa Madini Ya Makaa Ya Mawe , Serikali Ya Kijiji Itaimarisha Ulinzi Eneo Hilo Ili Kutosababisha Madhara Kwa Wananchi.
Akiwa Katika Eneo La Madini Yanayowaka Moto Kitongoji Cha Ulamba Kijiji Cha Usita Mkoa Wa Njombe Mjiolojia Wa Madini John Maganga Ameshauri Wananchi Kutofanya Shughuli Za Kuzarisha Mkaa Katika Eneo Hilo Wakati Ofisi Yake Ikiendelea Na Uchunguzi Wa Madini Hayo.
Eneo Hilo La Madini Limedaiwa Kuanza Kuonekana Moto Unawake Tangu Mwaka Jana Mwezi Wa Nane 2016 Hadi Sasa Hivi Bado Linaendelea Kuwaka Moto Ambapo Watalamu Wa Madini Wanatafuta Mbinu Za Kuuzima Moto Huo Ndiyo Maana Wamezuia Shughuli Za Kijamii Kuendelea.
No comments:
Post a Comment