BAADHI YA WASHIRIKI WA SEMINA YA WATALAAMU WA TFDA WAKISIKILIZA KWA MAKINI ELIMU INAYOTOLEWA NA WATALAAM TOKA KANDA.
AFISA AFYA MKOA WA NJOMBE MATHIAS GAMBISHI AKICHANGIA HOJA
HAWA NI WASHIRIKI WA KUTOKA HALMASHAURI ZA MKOA WA NJOMBE AMBAO NI WATALAAM WA AFYA,MAAFISA BIASHARA, MAAFISA KILIMO, ASKALI WA POLISI NA WADAU WENGINE WA TFDA
MENEJA TFDA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI BWANA Rodney Alananga
MUWAKILISHI WA MKURUGENZI MKUU WA TFDA DKT SIKUBWABO NGENDABANKA AKIZUNGUMZA NA WASHIRIKI WA SEMINA HIYO
AKIHITIMISHA SEMINA HIYO YA SIKU MBILI KAIM MGANGA MKUU SAMSON SORO SASI
NJOMBE
Watalaamu Wa Mamlaka Ya Chakula Na Dawa TFDA Waliopo Kwenye Halmashauri Wametakiwa Kujenga Tabia Ya Kutoa Taarifa Kila Mwezi Za Kazi Wanazofanya Za Utafiti Na Ukaguzi wa Maduka Katika Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Ili Kutambua Mambo Muhimu Yanayotakiwa Kufanyiwa Kazi.
Rai Hiyo Imetolewa Na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Dkt Samson Soro Sasi Wakati Akifunga Mafunzo Ya Siku Mbili Kwa Watalaamu Mbalimbali Wanaounda Kamati Ya Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Katika Halmashauri Mkoani Hapa.
Dkt Soro Sasi Amesema Kuwa Kwa Kipindi Chote Kumekuwa Na Changamoto Ya Baadhi Ya Watalaamu Mbalimbali Wa TFDA Kutoa Taarifa Pindi Wanapokuwa Wamefanya Kazi Ya Ukaguzi Kwenye Halmashauri Zao Licha Ya Kufanya Kazi Ili Kuwawajibisha Watakaokiuka Utaratibu Huo.
Dkt Soro Sasi Ametaka Washiriki Wa Mafunzo Hayo Yalioandaliwa Na Mamlaka Ya Chakula Na Dawa TFDA Kwa Watalaamu Wake Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Kutumia Kikamilifu Kama Walivyokumbushwa Kwenye Mafunzo Hayo Ili Kutoa Elimu Kwa Wafanyabiashara Na Wananchi Juu Ya Kutumia Vyakula Vilivyopitwa Muda Wake Wa Matumizi Ya Binadamu.
Akizungumza Mara Baada Ya Kuhitimishwa Kwa Mafunzo Hayo Meneja Wa Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini Rodney Alananga Amesema Mafunzo Hayo Yatasaidia Watalaamu Hao Kufuatilia Majengo Ambayo Hayajasajiliwa, Na Kutoa Elimu Kwa Wananchi Huku Wananchi Nao Kuonesha Ushirikiano Kwa TFDA Ili Kutoa Huduma Bora Ya Chakula Na Dawa.
Nao Baadhi Ya Washiriki Wa Mafunzo Hayo Wameshukuru Kwa Elimu Iliyotolewa Kwani Kuna Baadhi Ya Mambo Yanayohusu Uingizwaji Wa Bidhaa Zisizosajiliwa Ambapo Sasa Watakwenda Kugundua Badhaa Bandia Na Zisizobandia Ili Wananchi Wapate Huduma Ya Chakula Kilicho Salama.
Katika Mafunzo Hayo Yaliotolewa Kwa Siku Mbili Yamewahusisha Wakaguzi Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Wakiwemo Jeshi La Polisi,Maafisa Afya, Maafisa Biashara,Kilimo Na Mifugo, Wafamasia,Wanasheria, Wahasibu Na Waganga Wakuu Wa Halmashauri Za Wilaya.
No comments:
Post a Comment