KATIBU TAWALA MSAIDIZI MKOA WA NJOMBE JOSEPH MAKINGA AKIWA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE ,CHRISTOPHA OLE SENDEKA KWENYE SEMINA INAYOENDELEA KATIKA UKUMBI WA NURSING KIBENA
NJOMBE
Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Nchini TFDA Imeanza Kutoa Semina Ya Siku Mbili Kwa Watalaamu
Wake Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Ili Kukabiliana Na Tatizo La Wafanyabiashara
Wanaoendelea Kuwauzia Wananchi Vyakula Vilivyopitwa Muda Wake .
Akizungumza Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Christopha Ole Sendeka ,Katibu Tawala
Msaidizi Joseph Makinga Amesema Halmashauri Zimekuwa Zikisajiri Kwa Kasi Ndogo Majengo
Yanayojihusisha Na Bidhaa Zinazodhibitiwa Na Mamlaka Ya Chakula Na Dawa TFDA Na Kusema
Semina Hiyo Itasaidia Kuongeza Kasi Ya Usajiri Huo.
Makinga Amesema Kuwa Katika Utaratibu Wa Serikali Hakuna Mtu Anayeruhusiwa Kufanya Biashara
Ya Kuzarisha,Kufanya Biashara Ya Kutunza Na Kuuza Bidhaa Zinazodhibitiwa Na TFDA Katika Jengo
Ambalo Halijasajiliwa Na Kwamba Kwa Majengo Yaliosajiliwa Yanatakiwa Kukarabatiwa Au Kufungwa.
Bwana Makinga Amebainisha Majengo Yaliosajiliwa Na TFDA Kwa Mkoa Wa Njombe Ni Machinjio
Matatu Tu Yaliosajiliwa Ambapo Amesema Maduka Ya Nyama Yani Bucha , Mighahawa Na Machinjio
Ni Machafu Na Kuhatarisha Afya Za Walaji Na Kuzitaka Halmashauri Kufanya Ukaguzi Wa Mara Kwa
Mara Katika Vituo Vya Kutolea Huduma.
Kwa Upande Wake Muwakilishi Wa Mkurugenzi Mkuu TFDA Taifa Ambaye Ni Mratibu Wa Ofisi Za
Kanda Na Halmashauri Dkt Sikubwabo Ngendabanka Amesema Kazi Ya Watalamu Wa TFDA Ni
Kutoa Ushahidi Na Ushauri Wa Kitalaamu Pale Anapobainika Mtu kula Chakula Kisichostahili Na Hatua
Nyingine Za Kisheria Kuchukuliwa.
Nao Washiriki Wa Semina Hiyo Wamesema Wanaamini Kuwa Semina Hiyo Itakwenda Kuwajengea
Uwezo Na Mbinu Za Kufuatilia Bidhaa Ambazo Hazitakiwa Kwa Matumizi Ya Binadamu Nakwamba
Semina Hiyo Itawafungua Ufahamu Wa Kubaini Makosa Yalipo.
Semina Hiyo Ya Siku Mbili Inalengo la Kukumbushana Namna Bora Ya Kusimamia Na
Kupeana Taarifa Za Udhibiti Kwenye Ngazi Ya Halmashauri Ili Wote Watafute mbinu Na Njia Sahihi Za
Kukabiiana Na Changamoto Zilizopo Ambapo Leo Semina Hiyo Inatarajia Kuhitimishwa.
No comments:
Post a Comment