MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman
Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.
Maombi
hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua
si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.
Uamuzi huo wa majaji umefikiwa
kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali
Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana
msingi kisheria.
Katika hatua nyingine, mwanahabari
nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu
Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.
Mbowe amefungua kesi hiyo ya
kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
Maombi
hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua
si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.
No comments:
Post a Comment